Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 30 August 2012

MSINIITE MZEE MAGARI.


Nyota kwenye tasnia ya filamu nchini Charles Magari amekataa kuitwa mzee while age yake imeshasogea.
Hali hiyo ilitokea hivi karibuni baada ya wasanii chipukizi kumpa jina la 'mzee' kutokana na ushauri wake anaowapa wasanii hao kwenye tasnia hiyo.

"Mimi sitaki kabisa kusikia mtu ananiita mzee wakati ni kijana, nashangaa kila nikipita mitaani naitwa mzee waambieni na wengine silitaki jina hilo”, Mzee Kijana Magari.

Pia mzee Magari alisema kuwa yupo mbioni kuzindua filamu yake inayoitwa "Zig Zag" iliyoandaliwa na Pilipili Entertainment, mbapo ndani yake kutakuwepo na vichwa kama Haji Adam na Mohamed Fungafunga.

MWAKA WA SHETANI KWA MAY D, YOU TUBE ACCOUNT YAKE YAFUTWA


We all know that May D hivi sasa hayupo tena chini ya label ya Square Records, leboiliyokuwa isimamia kazi zake hadi hivi majuzi alipotimuliwa.
Kwa upande mwingine inashtusha kusikia kuwa official YouTube channel ya singer huyu liyokuwa ikisimamiwa na Iroko Partners imefutwa siku mbili zilizopita pamoja na video zake za "Soundtrack" na "Ile Ijo".
Pamoja na videos za nyimbo hizo, page nyingine zilizotolewa ni pamoja na  streams za still clips.
Square Records’ Youtube accounts pia zinasimamiwa na Iroko Partners.
Hadi sasa haijawekwa wazi iwapo ni  Square Records, Iroko au hata  May D mwenyewe aliyeamua kuifuta account hiyo.
Infoz za kuaminika zinadai kuwa hadi sasa hakuna e-mail hata moja iliyotumwa kwa Iroko na pia Square records kuulizia issue imeibiwa.
Kwenye recent interviews Psquare waliweka wazi kuwa kuondoka kwa May D kwenye label hiyo kutamfanya kuwa na ya kujibu kiuongozi zaidi.

GADNER HUYO TIMES FM ATAKUWA AKITANGAZA SHOW IITWAYO MASKANI




Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, Garder G Habash aka Captein anatarajia kuanza kutangaza tena Jumatatu ijayo kupitia kituo cha radio cha Times FM 100.5 cha Dar es Salaam kwenye kipindi cha .
"Maskani" kitakachokuwa kikiruka from Jumatatu to Ijumaa saa 10 jioni hadi saa 1 usiku.


Gadner akiongea machache baada ya kutambulishwa Times FM
  Rumors dong the rounds ni kuwa mtangazaji huyo atakuwa akilipwa shilingi milioni 5 kwa mwezi na kama tetesi hizi zitakuwa ni za kweli basi Gadner atakuwa the most paid radio personality in Tezee.





Kipindi chake kinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na kipindi chake cha zamani,  Jahazi cha Clouds FM ambacho kwa sasa huendeshwa na Arnord Kayanda, Wasiwasi Mwabulambo na Ephraim Kibonde.

Hata hivyo Clouds FM watakuwa na advantage katika mikoa mingine ambayo Times FM haisikiki.

Picha ya pamoja ya baadhi ya watangazaji wa Times FM. Kutoka kushoto ni: Gadner, Schola, Natasha, Ndimbo, Dida na Joet.
Kwa upande wa Dar es Salaam, Maskani ina nafasi kubwa ya kuchukua wasikilizaji wengi wa Jahazi hasa wanaosikiliza radio wakiwa majumbani.

Times FM wana disadvantage ya frequency walinayo ya 100.5 ambayo gari nyingi haizifikii na hii ni kwa sababu kuna wasikilizaji wengi jijini Dar es Salaam wanaosikiliza radio kwenye magari.

ITAZAME OFFICIAL REMIX YA WIMBO WA MATAPELI WA JAGUAR

MAANDALIZI YA SEND OFF YA AUNTY EZEKIEL UTATA MTUPU




Zimepita week kadhaa toka kikao cha Aunty Ezekiel kifanyike nyumbani  kwake pamoja na Wajumbe wenzake wa tasnia ya filamu hapa nchini inayofahamika kama Bongowood.
 Kikao hiki cha Aunty Ezekiel kimezua utata baada ya kila mjumbe kutoa ahadi katika kikao cha kwanza na kutokufika katika kikao cha pili hii iliwashangaza watu wengi sana hasa ndugu na marafiki mbalimbali waliofika katika kikao hicho.
Asilimia nyingi ambao waliotoa ahadi ni wasanii wenzake na inasemekana kwamba muhusika wa maandalizi haya ya send off  yuko ziarani. Je huu si utata?.

SENE TA JEMBE Final HD teaser new

MJENGO MPYA WA MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE


  Muonekano wa mbele wa hekalu la Mchungaji Rwakatare
 MC na mchungaji Haris Kapiga wa Clouds FM
 Mc Harris Kapiga akiwa kazini.
Watu wakijiachia
  Kabati la vyombo 
 Akiwa katika ofisi yake ya nyumbani, kuna sehemu ya kufanyia mikutano, Salon, Studio, na sehemu ya mazoezi.
Wadau wakijiachia kwenye moja wapo ya kochi  la kifahari mjengoni humo
 Wakati wa msosi
 Mambo ya dressing table
Kitanda chake cha kulalia
---
 Mchungaji Getrude Rwakatare amehamia rasmi katika nyumba yake mpya iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya Hindi. Inaripotiwa kuwa waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika mahali hapo kwa kushuhudia nyumba yake hiyo ya kifahari.
 
Kabla ya kuhamia kwenye hekalu lake jipya Mch. Mh. Getrude Pangalile Rwakatare alikuwa akiishi Mikocheni B katika nyumba nyingine ya kifahari pia.

Images via Ruma Africa

Wednesday 29 August 2012

MARTIN KADINDA KWENDA KU-SHOWCASE DESIGNS ZAKE MAREKANI KWENYE AFRICA NEW YORK FASHION WEEK

Hard work pays.

Baada ya kufanikiwa kuwateka fashionistas wa Bongo kwa designs zake za Single Button na Vibunduki  now Martin  Kadinda is going to places baada ya kupata mwaliko wa kwenda kuonyesha brand zake huko New York kwenye Africa New York Fashion Week itakayofanyika August 31 mwaka huu.

 
"Kwa mara ya Kwanza Maishani mwangu nitakanyaga Ardhi ya Marekani Ijumaa hii, nitakuwa the only Designer Mwalikwa katika Africa New York fashion...... Kivumbi collection itaonekana tena ndani ya New York.. kivumbi collection Hiyoooo.. single button hizooo and Ofcourse Vibunduki teheheteetehehehhe"-said Martin Kadinda.
 

CHECK IT OUT: MIRIAM ODEMBA NEW LOOK

TUNDA MAN - DEMU SIO (OFFICIAL VIDEO PART 2 )

GUESS WAT...SUBIRIA VIDEO MPYA YA WIMBO WA MABESTE FT.JUX - SIRUDI TENA





 



BRAND NEW SONG FROM CHID BEENZ - MSHAMBA FEAT. SHARO MILIONEA

 


KWELI DIAMONDS ARE FOREVER - KUPIGA SHOW MAREKANI TAREHE 1 SEPT.


KWA MARA YA KWANZA KABISA NDANI YA MAREKANI..DIAMOND LIVE IN WASHINGTON DC JUMAMOSI HII TAREHE  1 SEPT!

FAT JOE - PRIDE N JOY FEAT. KANYE WEST (NEW VIDEO)

KAT DELUNA NEW VIDEO - WANNA SEE U DANCE (LA LA LA)

JESUS KUNOGESHA TAMASHA LA USIKU WA SAUTI NA MARAFIKI WA KWELI


Mwezi ujao kiongozi wa zamani wa Diamond Musica aitwaye Kibinda Nkoi aka Ibonga Katumbi 'Jesus' na  baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi wataungana kwa ajili ya kupagawisha mashabiki watakaojitokeza kwenye onesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.

Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ambaye anatamba na brand zake mpya ya ‘Single Button’na 'Vibunduki' alisema onesho hilo linawahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana na Jesus pamoja na hao wa Diamond, “Kila kitu kinakwenda sawa aliyekuwa amealikwa kwenye onesho hili ni Jesus,lakini kwenye onesho hilo atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa Diamond na Beta Musica kwa hali hiyo alishauriwa awaite wenzake ili wamsindikize”

“Kutokana na heshima waliyojengana na wenzake walikubali kumsindikiza kwa hiyo mashabiki wa Kibinda Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga Katumbi, Richard Mangustino, Wayne Zola Ndonga, na Alain Mulumba Kashama wakisimamia pamoja na kuimba tena nyimbo zao kali” alisema Kadinda


Aliongezea kuwa lengo kubwa la onesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha matumizi ya vyombo vya muziki, katika onyesho hilo pia watakuwepo wapiga magita kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga, Marcis Mengina na  mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound kwa jina la Kata Nyama Serikali.

   

Tuesday 28 August 2012

USAILI WA MAISHA PLUS SEASON MPYA WAANZA

Zoezi la kwasaka watu watakaoweza kuingia kwenye shindano la Maisha Plus, imeanza jana (Agosti 27) huko Bagamoyo mkoani Pwani...

Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe

Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili utafanyika Karatu

Agosti 31 – Singida
Usaili utafanyika Singida Mjini

Septemba 1- Iramba
Usaili utafanyika Iramba Mjini

Septemba 2- Dodoma
Usaili utafanyika Kondoa Mjini

Monday 27 August 2012

P SQUARE WAKIWA NA RICK ROSS UK KWENYE AFROBEAT FESTIVAL

KANYE AMFANYA KIM K KUBADILI NGUO ZAKE ZOTE


Kanye West anamtaka mpenzi wake Kim Kardashian avae mavazi ya heshima na ya kuvutia.


Katika kipindi cha jana cha Keeping Up With the Kardashians, rapper na mbunifu huyo wa mavazi, 35 – ameweka deal na mpenzi wake huyo wa miezi mitano kuwa kama atazitupa nguo zake zote atamnunulia zingine.

BBC DIRA YA DUNIA KURUKA LIVE LEO KWENYE TV

Saleem Kikeke

Matangazo ya televisheni ya Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC leo yanaanza kuruka rasmi kupitia Star TV ya Tanzania na Qtv ya Kenya.

Wiki iliyopita kulifanyika uzinduzi wa matangazo hayo jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo ya Dira ya Dunia kwa upande wa radio ni maarufu zaidi pengine kuliko matangazo yote ya radio za kimataifa zinazotangaza Kiswahili duniani.

Kuingia kwenye matangazo ya runinga kwa BBC Swahili kunafungua ukurasa mpya wa matangazo ya aina hiyo ya Kiswahili nchini.

BBC Dira ya Dunia siku za usoni itakuwa ikishindana na matangazo mengine ya Kiswahili ya Al-Jazeera ambayo yapo kwenye mchakato wa kuanzishwa.


CHIWAWA WA KENYA AZINDUA MAJI YAKE



Rapper wa Kenya aliyewahi kutamba na ngoma kali iitwayo ‘Mnafeel aje’, Chiwawa amezindua maji yake ya kunywa.

Maji hayo yanaitwa Minerva jina la kigiriki la mungu wa busara aliyekuwa akihusishwa na maji katika sehemu ya story zake.

Kwa upande wa Tanzania, Lady Jaydee aliwahi kujaribu kuanzisha maji yake lakini hata hivyo hayakuendelea kutolewa kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

SINTA APIMA NGOMA



"zoom ,,,,, tena zoom halafu hii ndio habari ya blue monday"

"Sisemi nao eeh,sisemi nao wanao comment mbofu mbofu kuhusu jlo,,
Waganda hapa wangesema nakowaaaaa, maana mtoto wa watu sili silali sihemi
sina la kusema zaidi, mimi huwa ninafanya vitendo tu,, Je wewe umepima? au kazi kushadadia ya watu,,, haya zueni balaa lengine hili naona mmeloana na macho yamewatoka kama fundi saa akiangalia mishale kama iko sawa.
Kama nawaona mlivyokuwa na hasira n comment lolest."

NEW SONG FROM PAH ONE -ASAMBEENI




MDOGO WAKE KANUMBA ARITHI MIKOBA YA KAKA YAKE


Ni miezi kadhaa imepita sasa tangu kifo cha one of the best actor ever in Tzee film industry kwa jina la Steven Kanumba kitokee. Na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kusema kampuni ya Kanumba The Great itakuwa inafanya kazi chini ya usimamizi wa Seth Bosco na Abela au Mrs Bile ambae ni dada yake na Marehemu Steven Kanumba ambae Kanumba ndio alikua anamfata kwa kuzaliwa.
Latest infoz nikuwa company hiyo  imeshakamilisha movie mpya kwa jina la “Malaika” ikiwa imeshirikisha wasanii km Rose Ndauka, Abdalah Mkumbila, Seth Bosco na Kijana Rammy Galis ambaye anatarajiwa kuwa Kanumba part 2 kutokana na muonekano wake kufanana na The late Steven Kanumba.
Filamu hii inatarajiwa kuwaburudisha mashabiki wa Kanumba na itasambazwa na Steps Entertainment LTD , kaa mkao wa kula kijipatia Copy yako pindi itapokuwa madukani.

Friday 24 August 2012

R.I.P MATONYA




Yule ombamba maarufu kuliko wote nchini , Matonya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

“Namtaarifu Komredi Yusufu Makamba, kuwa yule kiboko yake 'MATONYA' amefariki usiku wa kuamkia leo kijijini kwakwe Mpamantwa wilaya ya Bahi, mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni kijijini hapo. Habari ziwafikie, Mkuu wa Wilaya Betty Mkwasa, Familia ya Mzee Makamba popote walipo, wakazi wa Dar na Moro pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote. Bila ya kusahau wale wa eneo la Darajani Mjini Morogoro", ameandika mwandishi wa habari Habel Chidawali ambaye amewahi kumfanyia mahojiano ombamba huyo.

Matonya amefariki akiwa anaishi kwenye nyumba ya tembe ambayo ni mali  ya mtoto wake wa kike aitwaye Elizabeth Matonya.

Nyumba hiyo ya asili ya watu wa Dodoma ipo kwenye Kijiji cha Bahi Sokoni katika Kitongoji cha Nghungugu, umbali wa kilomita 3 kutoka yalipo makao makuu ya wilaya ya Bahi.

Katika mahojiano aliyofanya na Habel, Matonya enzi za uhai wake alisema kuwa hana mali yoyote kama wengi walivyokuwa wanadhani.

“Watu wanasema kuwa nina mali, lakini ni ‘walambi’ (akimaanisha kwamba ni waongo). Mimi sina kabisa mali; hata mbuzi; hata kuku sina na wala sina mpango wa kununua tena hata kama nina pesa kwa kuwa walishazoea kuniibia, hivyo sitaki tena kuwa na mali.”

Nilikuwa na ng’ombe wengi sana. Kila wakati walikuwa wakiwaiba wakati ninaishi Kilimatinde na ng’ombe hao nilinunua kwa pesa yangu ya kuomba huko Dar es Salaam. Walikuwa wengi lakini waliibwa wote na ndugu zangu.

Kuhusu kuacha kuomba

Jibu: Labla serikali inijengee nyumba nzuri hapa na inipe mtu wa kunitunza au hata wakijenga nyumba nzuri kwa mtoto wangu halafu wanisaidie na chakula pamoja na chai ya kila siku, mimi naweza kustaafu kazi yangu lakini bila ya kufanya hivyo kazi yangu nitakufa nayo.

Katika mahojiano hayo Matonya alisema alikuwa akipata kati ya Sh50,000 hadi 100,000 kwa mwezi na mara nyingi alikuwa akirudi kijijini kila baada ya miezi miwili au mitatu tangu alipoanz`a kazi hiyo mwaka 1961.

Rest in Peace Matonya.

ANA PETER WA EA RADIO AJA NA WIMBO WA " A CALL"


Mtangazaji wa show ya Power Jams ya East Africa Radio, Ana Peter ameachia ngoma mpya yenye mahadhi ya reggae iitwayo "A call".

Ngoma hii imetengenezwa na DX wa Arusha kwa kutumia beat ya riddim ya "heart & soul riddim".

"Nimeimba kuhusu kufata ndoto zetu katika maisha,kuondokana na dhana potofu kuwa maisha yana formula fulani.Shule ni muhimu sana katika kuturahisishia maamuzi maishani,Pasipo uelewa na maarifa,Maisha huonekana magumu zaidi,Matumizi ya vilevi kupita kipimo ama hata kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya yote ni matokeo ya kupuuza malengo endelevu na kufata mikumbo, anasema Ana.

"A call ni inspirational reggae song ambayo kwa haraka ni rahisi kuiweka katika category ya Gospel ambayo ni sawa pia,kwani kazi yangu kama artist, especially wa kike kuelimisha vijana wenzangu.Enjoy and support Tanzanian Music."

BEN POL NEW SINGLE-PETE

Pete  ni wimbo wa kwanza wa Ben Pol tangu aachie albam yake iitwayo Maboma akiwa chini ya MLab. Kwa maana nyingine ni kuwa huu ndio wimbo mpya aliorekodi akiwa nje ya label ya MLAB. 

"Thank God it's been a great journey and I personally feel the singles of that album were great. I have now come with a new production team and heading for my second album. Share it and I hope you enjoy this record as much as I enjoyed recording it. Peace and much love," ameandika Ben kwenye maelezo yake.

Wimbo huu umendikwa na waandishi watatu akiwemo yeye mwenyewe Ben Pol, Fred Max na Lady Peace Winnie.. Producer ni Mona Gangsta wa Classic Sounds.


Mashairi

Verse 1;

Hadithi ya penzi langu umenikata nini mwisho
huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho
 nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, nishawahi kukosa
nasema niliteseka mchana na usiku mimi
nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, sitaki tena kosa
najua nitateseka
mwisho sitokuwa nawe tena naulizaa
Chorus;

Kama pete yangu, inakuchomaa kidoleni
ni kama pendo langu , linakuchoma moyonii ,
bora kuitoa aaah aah ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
bora kuitoa aaah aa ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
Verse 2;

sikujali wambea wanafki walosema
hatutadumu mimi nawe tutajaachana
wakiniona siko nawe si ndo watasema
hata nyumbani watajua tumefarakana
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
kila jema n'tendalo mie ,kwako limekuwa sio
nitakapo kujua ulipo ,wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako ,yanisuta mwenzio
ndo maana nikukosapo ,moyo wanienda mbio

Thursday 23 August 2012

CHECK OUT RICK ROSS AKI-PEFORM KWENYE SUMMER JAM CONCERT HUKO NIGERIA

EXCLUSIVE: K LYNN IS PREGIOUS

Mama kijacho


List ya baby boom kwenye Miss Tanzania inataongeza siku si nyingi.
Baada ya Hoyce Temu, Nagris Mohammed, Miriam Gerald, Silvia Shally na Nancy Sumari ambao waliwahi kuwa mamiss Tezee kumuongezea Uncle Lundenga cheo cha U-uncle baada ya kujaliwa watoto,  latest news ni kwamba Jacquline Ntuyabaliwe better known as K Lynn naye yuko mbioni kuongeza mjomba mwingine coz she's now eating for two.



Habari za uhakiaka zinadai kuwa jamaa mwenye makampuni MEEENGI hapa nchini ndiye aliefanikisha zoezi hilo.

P SQUARE NEW AUDIO - ALINGO

MB DOGG KWENYE MOVIE


Filamu kali na ya kusisimua ya Nankonda wa Mikindani inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni ndio itakayokuwa filamu ya kwanza kumtambulisha msanii wa  Bongo fleva  kwa jina la Mbwana Mohamed  aka ‘Mb Dogg’ kuingia katika tasnia ya filamu.
Filamu hiyo ambayo Mb Dogg amacheza kama mhusika mkuu imetayarishwa na Dr. Cool Production company.
 “Uwezo alionyesha Mb Dogg ni wa hali ya juu sana, utafikiri alikuwepo katika tasnia ya uigizaji kwa miaka mingi , msanii amebeba uhusika kulingana na hadithi yenyewe nasema ni msanii anayejua kuigiza na hilo mtalismtalishuhudia katika filamu hiyo,” said Mzee Korongo.

NYUMBA MPYA YA CEO WA CASH MONEY

Ronald Williams Aka Slim ambaye ndio C.E.O Wa Cash Money ndiye amenunua nyumba ya thamani ya Dollar zaki Marekani Milliom $ 7.15. Ni Nyumba yenye vyumba 9 vya kulala ,Mabafu 12. 
Unuunnuzi wa nyumba hii umekuwa wa siri sana kitu ambacho ni tafauti na wasanii wa kundi hilio la Cash Money huwa wanapenda kutangaza mambo yao yote ya thamani. Ronald ni kaka wa Bryan 'Birdman' Williams na ni mmoja wa wadau matajiri sana kwenye mziki Marekani mwenye Thamani ya Dollar za Kimarekani Million $100



CHECK THIS OUT...IS KANYE A BODYGUARD TO KIM?