Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday 9 April 2013

AVRIL KUUZA MADAWA YA KULEVYA!

Singer now turning to be an actress Avril amekula mchongo wa ku-act katika tamthiliya ya 'Noose of Gold’ inayorushwa na kituo cha M-NET. Avril ataigiza katika season ya 5 ya tamthiliya hiyo na nafasi yake ni ‘Muuza madawa ya kulevya’.

Avril alipoulizwa kama nafasi hiyo inaakisi maisha yake ya kawaida ya kila siku, alikana kwa kusema, “Sijawahi kuhusika iwe kwa kutumia au kuuza madawa ya kulevya. Sasa hivi ndio najifunza mambo haya”.

Pengine nafasi hii imekuja baada ya kuonekana amefanya vizuri sana kiuigizaji katika video ya 'Kesho' ya Diamond.
 

 
 


RAISI WA URUSI AONYESHWA MATITI ZIARANI HADHARAN!


Raisi wa Urusi Vladimir Putin na Chancellor wa Ujerumani, Bi. Angela Merkel walikutana na kimbwanga cha mwaka baada ya kuvamiwa na mwanamke mwanaharakati aliyeku wazi kabisa kifuani na kuwaonyesha matiti yake viongozi hao walipokuwa katika ziara ya viwanda huko Hanover, Ujerumani jana Jumatatu.



Hata hivyo Bi. Angela Merkel hakufurahishwa na ulinzi mbovu hivyo kumruhusu mwanamke huyo kujipenyeza mpaka kuwafikia viongozi hao!


Cheki reaction ya bwana raisi baada ya kuonyeshwa matiti.

KANYE WEST AIBA NGOMA!


Roc-A-Fella Records & Good Music Rapper Kanye West, 35, ameingia matatani kwa kuiba baadhi ya mistari na kuitumia katika ngoma yake ‘Gold Digger’. Jana Jumatatu Trena Steward na Lorenzo Pryor, watoto wa David Pryor, ndio waliofungua kesi hii kwa niaba ya baba yao aliyeimba wimbo huo 'Bumpin Bus Stop' kwa kushirikiana na bendi yake, Thunder & Lightening mwaka 1974.
 
Ni sekunde 13 tu za wimbo wa David Pryor  ndio West alikopi mistari pia tune ambayo ni 'Get down' three times’ huku West alisema, 'Get down, girl, go head get down' three times’. Trena Steward na Lorenzo Pryor, watoto wa David Pryor kila mmoja anamiliki robo ya tune katika wimbo huu na wanahitaji fidia ya $ 150,000 pamoja gharama za wakili.

Hii sio mara ya kwanza kwa West kupelekwa mahakamani kwani  mwaka September, 2012, New York record label, TufAmerica ilimfungulia mashtaka West kwa kuchukua mistari ya ngoma ya Eddie Bo,  'My Beautiful Dark Twisted Fantasy' na kutoa ‘Stronger’.