Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday 15 January 2013

AMBER ROSE KITAMBI HADHARANI

Zikiwa zimebaki siku chache aitwe mama, Amber Rose ameonekana kitaani akienda zake saluni (sio ya Salama katika Mkasi), kutengeneza kucha na nywele jijini Los Angeles, huku kitumbo chake kikionekana wazi, jana Jumatatu!

"Leo ni siku ya kwanza kuanza masomo yangu ya uzazi hapa nyumbani. Hakuna bekitatu wala hospitali, nataka iwe siri ndani ya nyumba yangu. Nimefurahishwa na uzoefu huu", aliandika Amber katika akaunti yake ya twitter siku kadhaa zilizopita huku zikisalia very few days she and Wiz Khalifa kukikaribisha kiumbe chao kipya duniani - a baby boy!

Dizaini kama the X-boyfriend wa Amber, KW, hakuwa akiifanya kazi yake ipasavyo!!!





NICKI MINAJ ANYWEA KWA MARIAH CAREY

The Young Money lady rapper Nicki Minaj atangaza rasmi kufuta bifu kati yake na Mariah Carey, katika interveiw na Ellen DeGeneres itakayorushwa Jumanne(leo). Hii ni baada ya Nicki kuchaguliwa kukaa pamoja na Carey katika panel ya majudge ya American Idol. 

"Nilisikia stuff wenzangu chote walichosema na sikuweza kuamini. Niliwasikia wakisema kuwa Carey hanitaki katika jopo la majaji. Lakini nikajisemea kuwa mbona mimi na Carey ni marafiki!", alifunguka Minaj.

    Nicki Minaj na Ellen DeGeneres katika interview.

 
American Idol Judges; Randy Jackson, Mariah Carey, Keith Urban, Nicki Minaj na mshereheshaji Ryan Seacrest!