Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday 4 May 2013

JUSTIN BIEBER ASIMAMISHA SHOW KUPISHA SWALA

Kipenzi cha walimbwende, Justin Bieber juzi Alhamiis alisimamisha show yake ili kupisha waumini wa dini ya Kiislamu kuswali (Waumini wa dini hiyo huswali mara tano kwa siku). Na baada ya swala dogo aliendeleza makamuzi kama kawaida. Hii ilitokea jijini Istanbul, Uturuki katika concert iliyofanyika Technical University sports arena.
Kupitia akaunti mbalimbali twitter za mashabiki wake walipendezeshwa na tukio hilo na kuandika hivi:-
Photo - Justin Bieber Stops Concert For Muslim Prayer
Pamoja na hayo bado Justin Bieber amekutana na vikwazo mbalimbali katika nchini za Kiarabu vikiwemo kufutwa kwa show yake huko Oman  kwa vile shows zake huchochea ngono kwa vijana!
 
 

JENGO LINALOFANANA NA UUME NCHINI CHINA.

Jengo hilo lenye urefu wa mita 150, hivi sasa bado linaendelea kujengwa jijini Beijing. Kutokana na muundo huo usiokua wa kawaida, picha za kibunifu zikaanza kuibuka katika website ambayo ni kama “Twitter ya China,” inayoitwa Sina Weibo.

Watu wengi wameeleza kuwa kwa kutumia ubunifu kidogo tu wa photoshopping, unaweza kuambatanisha picha ya jengo hilo, ambalo raia wamelipa nickname “Giant Penis” au “Uume mkubwa,” katikati ya “miguu” ya jengo lingine maarufu nchini humo ambalo ni makao makuu ya kituo cha TV cha China Central Television (CCTV,) almaarufu kama  “Big Underpants” building au Jengo la Chupi Kubwa.


Habari za utani huo zilifikia wakubwa nchini humo ambao walikerwa na kuamua kuwaharibia watu raha zao kwa kuamuru website ya Sino Weibo ku-block search zote zinazotafuta picha au habari za jengo hilo. Kwa sasa Wachina wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe “kuendana na sheria, kanuni na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search results) hayawezi kuonyeshwa.


Mwandishi wa Reuters Anita Li amesema “hii inaonyesha frustrations miongoni mwa vijana watumiaji wa internet nchini China, na pia inaonyesha ni kiasi gani “wakubwa” wako sensitive kwa hata vitu vidogo vya kipuuzi online.”