Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 16 August 2012

ALLY REHMTULLAH KUZINDUA DESIGNS ZAKE TAREHE 8 SEPTEMBER 2012

 
 
MWANAMITINDO  maarufu nchini, Ally Rehmtullah pichani juu atazindua onyesho rasmi la kazi zake mpya  za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanawake na wanaume ‘Ally Rehmtullah 2013 Collection’lililopangwa kufanyika Hoteli ya Serena,  jijini Dar es Salaam, Septemba 8 2012.
  Rehmtullah alisema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati za kuinua kiwango cha kazi za mitindo kwa Tanzania.
“Nimepania kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini,  ili kazi za wanamtindo na wabunifu ziweze kupenya kwenye soko la ndani na la Afrika Mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.
Pia aliongeza kuwa, kwenye uzinduzi huo mavazi na onyesho litapambwa kwa rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa mwafrika.
Aidha, Rehmtullah alisema licha ya kuonesha mavazi pia kutakua na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nyota, ambapo pia aliwataja wadhamini wakuu wa onyesho hilo kuwa, Mercedez Benz, Mo Blog, Belvedere Vodka, Dulux, Raha, Hugo Domingo,The Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, Quality Furniture na Mx Carter.
Katika onesho hilo, linatarajia kudhuriwa na watu 400, wakiwemo viongozi wa serikali, wafanyabiashara na wageni mbalimbali  ambapo watashuhudia wanamitindo wengine mahili na chipukizi watakaoonesha mitindo siku hiyo.

WAREMBO WA REDDS MISS ILALA WATAMBULISHWA LEO





Mratibu wa Shindano la Redd's Miss Ilala 2012, Gadner G. Habash akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge mchana huu wakati wa kutambulisha warembo watakaoshiriki kwenye fainali ya Redd's Miss Ilala 2012. Washindi watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012.Wengine Pichani toka Kulia ni Mratibu Mwenza wa Shindano hilo,Juma Mabakila, Cylivia Mashuda na Neema Mbula ambao ni walimu wa warembo hao.







Baadhi ya warembo watakaoshiriki Shindano la Redd's Miss Ilala wakiwa kwenye kikao hicho.



WASANII KUMI MATAJIRI ZAIDI ZAIDI BARANI AFRICA

Youssou Ndour


1. Youssou Ndour

Huyu ndiye mwanamuziki tajiri zaidi barani Africa. Jamaa anamiliki kituo kikubwa zaidi binafsi cha runinga nchini Senegal, kampuni ya magazeti na kituo chaa radio.

Anamiliki pia night club na record label. Anamiliki kampuni ya nyumba na makazi. Mwaka 2004 jarida la Rolling Stone lilimwelezea kama mwanamuziki maarufu zaidi nchni Senegal na pengine Afrika aliye hai.

Tangu April 2012, ni waziri wa utalii na utamaduni nchini Senegal.

Matumizi ya nyimbo zake yanamuingiza mamia kwa maelfu ya Euro!

2.P-Square

Hakuna msanii wa kizazi cha leo anaeweza kugusa matawi ya mapacha hawa, Peter na Paul Okoye. Wana hela chafu!

Wanachaji dola 250,000 kwa kila show ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 390 za Tanzania! Kuongezea msumari zaidi hapo ni kwamba hawa jamaa wana show kila weekend! Mpaka sasa hivi wameshafanyiwa booking ya kufanya show sehemu mbalimbali duniani hadi March mwakani!

Nyumba yao waliyoipa jina la Squareville huko Ikeja Nigeria ina thamani ya dola milioni 3 ambazo ni zaidi  ya shilingi bilioni 4.

Waliweka historia kwa kuwa wasanii wa kwanza kununua kiwanja kwenye eneo la Banana Island nchini Nigeria ambacho kina thamani ya zaidi ya dola milioni 3 pia!

Wana mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya pili kwa ukubwa ya simu nchini Nigeria ya Globacom wakiwa kama mabalozi wake ambapo hulipwa dola milioni 1 kwa mwaka, wanamiliki pia mijengo kibao ya kupangisha.
3.D'banj

Mnigeria huyu aliye chini ya label ya Kanye West, G.O.O.D Music, alitengeneza takriban dola milioni 5 kwenye kampeni ya rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Anamiliki jina la ‘Koko’ linalojumuisha klabu bora za Nigeria za KokoLounge, maji ya kunywa Koko Water na Koko Mobile.

Aliwahi kufanya reality show ya TV  iitwayo Koko Mansion na kulipwa dola milioni 1.

Anamiliki nyumba yenye thamani ya dola milioni 1.5 jijini Atlanta. Ni mwenyekiti mtendaji wa Dbanj Records na pia ana kampuni ya ulinzi iliyofanikiwa sana.

Yeye hucharge dola 100,000 kwa show.
4.Koffi Olomide



Mfalme huyo wa Lingala anacharge tabriban Euro 100,000  kwa show. Jamaa hupiga show nchini Ufaransa zinazojaza karibu watu 80,000  ambapo tiketi moja ni Euro 30 sawa na shilingi elfu 60.

Amekwishatoa albam zaidi ya saba ambazo zimemuingizia mamilioni ya dola.
5.Salif Keita

Anajulikana pia kama ‘Sauti ya dhahabu ya Africa’, ni miogoni mwa watu wanyenyekevu lakini matajiri sana barani Afrika.

Msanii huyo albino anamiliki kisiwa chake binafsi nchini Mali.

Anamiliki majumba na mali zingine nchini Ufaransa na Mali.
6. Fally Ipupa

Msanii huyu anajulikana kama ‘Mfalme mpya wa Lingala’ wa DRC. Kutoka kuwa mcheza show wa zamani wa Koffi Olomide, anasifika kwa kuleta usasa zaidi kwenye muziki wa Lingala.

Ameshakuwa balozi wa brand nyingi za nguo nchini Ufaransa, concerts zenye gharama na kuuza kopi kibao za albam zake.

7.2 Face Idibia



Msanii huyu wa Nigeria anamiliki nyumba za kupangisha zenye gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.

Hulipwa kuanzia dola 50,000 - 80,000 kwa show.

Anamiliki pia klabu ya usiku ya nguvu na biashara zingine zinazomuingizia hela nyingi.
8.Hugh Masekela



Huyu ni miongoni mwa wanamuziki wa Jazz wanaoheshimika zaidi barani Africa.  Anamiliki mobile studio yenye mafanikio makubwa nchini Botswana. Hushiriki kwenye matamasha makubwa duniani na huingiza mamilioni ya dola kutokana na mauzo ya albam zake.
9. Banky W

Anajulikana kama Mr. Capable pia. Banky W hufanya show mara tatu ama nne kwa wiki zinazomuingiza mshiko mrefu mno. Aliwahi kuwa balozi wa kampuni ya simu ya Estisalat ya Nigeria ambapo alitumika kwenye matangazo yake.

Kwa sasa ni balozi wa Samsung Mobile. Amewahi kufanya kampeni ya Coca Cola-Nigeria na Microsoft’s Anti-cyber Crime Initiative.

Kutokana na kuingiza hela nyingi amenzisha mradi kuwasaidia wasiojiweza kwa kuwalipia ada watoto wenye uwezo darasani chini ya Mr. Capable Foundation.

10.Chameleone

Mzee wa Valuvalu anafunga list kwa kuwa msanii mwenye hela zaidi kuliko wote Afrika Mashariki.

Anamiliki gari Cadillac Escalade yenye thamani kubwa, Mercedes Benz ML 320,  Super Custom, convertible na Premio.

Anaishi kwenye nyumba yenye gharama kwenye maeneo  ya wazito huko Seguku Hill kwenye viunga vya Kampala, simu zake mwenyewe na mali zingine nyingi.

OBAMA ANA KIWANDA CHA BIA IKULU


Kuongoza nchi kubwa kama Marekani yataka moyo! Ndio maana Barack Obama aliamua kuwa na kiwanda cha bia kwenye ikulu ya White House ili kupunguza stress za cheo hicho kikubwa duniani. Isitoshe kipindi hiki ni kigumu kwake kwakuwa anaelekea kwenye uchaguzi, so kupiga mtungi si jambo la kushangaza kwake.


Amekuwa rais wa kwanza wa hivi karibuni nchini Marekani kunywa bia inayotengezwa kwenye Ikulu.


Bia inayotengenezwa humo imepewa jina la ‘White House Honey Ale’ ikiwa na rangi mbalimbali.

Asali kidogo inayopatikana kwenye bia hiyo inatoka kwenye mizinga ya nyuki anayofuga mkewe Michelle Obama kwenye bustani yao.

Video 11 za Bongo Flava zilizoangaliwa zaidi Youtube

 
 
Zifuatazo ni video 11 za nyimbo za Bongo Flava zilizotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube hadi leo hii.

1. Bushoke & Juliana Kanyomozi -  Usiende Mbali  1,301,132 views

2. Bushoke & K-LYNN - NALIA KWA FURAHA - 1,016,324

3. Xplataz – Nini dhambi - 949,865

4. Alikiba – Usiniseme -  927,777

5.Diamond – Mbagala 797,076

6. Tid – Nyota yako-   673,650

7. Diamond - Moyo Wangu - 666,346    

8. Alikiba -  Nakshi mrembo  - 605,520

9. MATONYA feat LADY J.D – ANITA - 483,943    

10. Professor Jay ft. Ferooz - Nikusaidiaje? - 414,634

11. Aslay - Nakusemea. 351,015

RUGE MUTAHABA KUHOJIWA KWENYE MAKUTANO SHOW YA JUMAMOSI HII

 
 
Wiki hii kwenye kipindi kipya cha radio cha Makutano Show kinachorushwa kila siku za Jumamosi kupitia Magic FM, mmoja wa mabosi wa Clouds FM Ruge Mutahaba atahojiwa na mtangazaji wa show hiyo Fina Mango.

Kwa namna yoyote interview hiyo itavuta wasikilizaji wengi hasa kwakuwa Fina atakuwa akimhoji bosi wake wa zamani  kipindi anafanya kazi Clouds FM.

Licha ya Fina Mango kuachishwa kazi pamoja na Masoud Kipanya, bado ameendelea kuwa karibu na Ruge ambao wanamiliki pamoja kampuni ya One Plus Communication.

Bila shaka itakuwa interview ya kuvutia.

ETI DULLY NDIYE MSANII WA KWANZA KUPANDA NDEGE BONGO?

 
 
Dully Sykes hajaacha tabia yake ya kujisifia ndo maana mama yake alimpa jina la Mr. Misifa. Akiongea na Clouds FM msanii huyo mkongwe amesema yeye ni msanii wa kwanza nchini kupanda ndege. Anasema anakumbuka ilikuwa mwaka 2000 alipanda ndege kuelekea Mwanza ambapo alikaa jirani na Joseph Kusaga ambaye alimwambia Dully  asiogope ndege kutokana na kuwa mgeni kwenye chombo hicho.

Dully pia ambaye kwa sasa ameongeza aka mbili ‘Superstar na Hunter’ amesema yeye ni superstar wa kwanza Tanzania baada ya Profesa Jay.

Amesema mwaka ambao Profesa aliachia wimbo wa Chemsha Bongo ndio mwaka aliotoa wimbo wake Julietha na kusema yeye ndiye aliyeitambulisha Bongo Flava nchini.

Aliongeza kuwa ameendelea kuwa pale pale na mafanikio yakiongezeka zaidi kutokana na kumheshimu kila mdau wa muziki bila kujali umri wake.