Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday 24 August 2012

R.I.P MATONYA




Yule ombamba maarufu kuliko wote nchini , Matonya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

“Namtaarifu Komredi Yusufu Makamba, kuwa yule kiboko yake 'MATONYA' amefariki usiku wa kuamkia leo kijijini kwakwe Mpamantwa wilaya ya Bahi, mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni kijijini hapo. Habari ziwafikie, Mkuu wa Wilaya Betty Mkwasa, Familia ya Mzee Makamba popote walipo, wakazi wa Dar na Moro pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote. Bila ya kusahau wale wa eneo la Darajani Mjini Morogoro", ameandika mwandishi wa habari Habel Chidawali ambaye amewahi kumfanyia mahojiano ombamba huyo.

Matonya amefariki akiwa anaishi kwenye nyumba ya tembe ambayo ni mali  ya mtoto wake wa kike aitwaye Elizabeth Matonya.

Nyumba hiyo ya asili ya watu wa Dodoma ipo kwenye Kijiji cha Bahi Sokoni katika Kitongoji cha Nghungugu, umbali wa kilomita 3 kutoka yalipo makao makuu ya wilaya ya Bahi.

Katika mahojiano aliyofanya na Habel, Matonya enzi za uhai wake alisema kuwa hana mali yoyote kama wengi walivyokuwa wanadhani.

“Watu wanasema kuwa nina mali, lakini ni ‘walambi’ (akimaanisha kwamba ni waongo). Mimi sina kabisa mali; hata mbuzi; hata kuku sina na wala sina mpango wa kununua tena hata kama nina pesa kwa kuwa walishazoea kuniibia, hivyo sitaki tena kuwa na mali.”

Nilikuwa na ng’ombe wengi sana. Kila wakati walikuwa wakiwaiba wakati ninaishi Kilimatinde na ng’ombe hao nilinunua kwa pesa yangu ya kuomba huko Dar es Salaam. Walikuwa wengi lakini waliibwa wote na ndugu zangu.

Kuhusu kuacha kuomba

Jibu: Labla serikali inijengee nyumba nzuri hapa na inipe mtu wa kunitunza au hata wakijenga nyumba nzuri kwa mtoto wangu halafu wanisaidie na chakula pamoja na chai ya kila siku, mimi naweza kustaafu kazi yangu lakini bila ya kufanya hivyo kazi yangu nitakufa nayo.

Katika mahojiano hayo Matonya alisema alikuwa akipata kati ya Sh50,000 hadi 100,000 kwa mwezi na mara nyingi alikuwa akirudi kijijini kila baada ya miezi miwili au mitatu tangu alipoanz`a kazi hiyo mwaka 1961.

Rest in Peace Matonya.

ANA PETER WA EA RADIO AJA NA WIMBO WA " A CALL"


Mtangazaji wa show ya Power Jams ya East Africa Radio, Ana Peter ameachia ngoma mpya yenye mahadhi ya reggae iitwayo "A call".

Ngoma hii imetengenezwa na DX wa Arusha kwa kutumia beat ya riddim ya "heart & soul riddim".

"Nimeimba kuhusu kufata ndoto zetu katika maisha,kuondokana na dhana potofu kuwa maisha yana formula fulani.Shule ni muhimu sana katika kuturahisishia maamuzi maishani,Pasipo uelewa na maarifa,Maisha huonekana magumu zaidi,Matumizi ya vilevi kupita kipimo ama hata kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya yote ni matokeo ya kupuuza malengo endelevu na kufata mikumbo, anasema Ana.

"A call ni inspirational reggae song ambayo kwa haraka ni rahisi kuiweka katika category ya Gospel ambayo ni sawa pia,kwani kazi yangu kama artist, especially wa kike kuelimisha vijana wenzangu.Enjoy and support Tanzanian Music."

BEN POL NEW SINGLE-PETE

Pete  ni wimbo wa kwanza wa Ben Pol tangu aachie albam yake iitwayo Maboma akiwa chini ya MLab. Kwa maana nyingine ni kuwa huu ndio wimbo mpya aliorekodi akiwa nje ya label ya MLAB. 

"Thank God it's been a great journey and I personally feel the singles of that album were great. I have now come with a new production team and heading for my second album. Share it and I hope you enjoy this record as much as I enjoyed recording it. Peace and much love," ameandika Ben kwenye maelezo yake.

Wimbo huu umendikwa na waandishi watatu akiwemo yeye mwenyewe Ben Pol, Fred Max na Lady Peace Winnie.. Producer ni Mona Gangsta wa Classic Sounds.


Mashairi

Verse 1;

Hadithi ya penzi langu umenikata nini mwisho
huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho
 nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, nishawahi kukosa
nasema niliteseka mchana na usiku mimi
nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, sitaki tena kosa
najua nitateseka
mwisho sitokuwa nawe tena naulizaa
Chorus;

Kama pete yangu, inakuchomaa kidoleni
ni kama pendo langu , linakuchoma moyonii ,
bora kuitoa aaah aah ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
bora kuitoa aaah aa ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
Verse 2;

sikujali wambea wanafki walosema
hatutadumu mimi nawe tutajaachana
wakiniona siko nawe si ndo watasema
hata nyumbani watajua tumefarakana
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
kila jema n'tendalo mie ,kwako limekuwa sio
nitakapo kujua ulipo ,wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako ,yanisuta mwenzio
ndo maana nikukosapo ,moyo wanienda mbio