Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday 17 August 2012

MAUNDA ZORRO AIBUKIA KWENYE MOVIE




Baada ya Maunda Zorro kuwa nje ya game yake kwa muda wa takribani miaka minne now she's back but round hii kwenye movie scene.
Kwa mujibu wa Maunda Zoro ni kwamba ukimya wake ulitokana na kuwa bussy location akiigiza movie inayptarajiwa kutoka hivi sasa kwa jina la  "
Room Number 13" chini ya kampuni ya ZG iliyopo Zanzibar ambayo ndani yake amecheza kama ghost.
Does that means anaacha mziki, "No siwezi kuacha mziki.Pamoja na kuwa kwangu kimya nilikuwa na-record ngoma ambazo management yake ilikuwa ikizizuia kuzitoa na hadi leo sijui inakuweje"-Maunda.

GELLY WA RHYMES'S NEW TRACK - MARRY ME



TRACK MPYA YA KIGWEMA - KWENYE MAGAZETI




NEW SONG FROM MR.NICE: KUPENDWA

OFFICIAL VIDEO FROM DULLY SYKES - MTOTO WA KARIAKOO

PUSH MOBILE WAKO TAYARI KUBORESHA MALIPO YA WASANII

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile Limited, Freddie Manento akizungumza na wanamuziki na wadau wake waliofika katika mkutano huo wa kujadili masuala mbali mbali ya biashara ya muziki nchini.
 
 Chart inayoonyesha malipo ya nyimbo za wasanii.


 Wasanii wakifuatilia.
 Producer Man Maji akifuatilia kwa makini.


 
Msanii maarufu wa bongo fleva, Ferouz akiwa na meneja wake Petee wakifuatilia mkutano huo kwa makini.
 
Mkutano huo ulijadili masuala mbali mbali ya kuboresha malipo ya wanamuziki hao ambapo Push Mobile Limited iliahidi kupigana kufa na kupona na wadau wake (kampuni za mitandao ya simu za mkononi) ili kuboresha malipo yao.
---
KAMPUNI ya Push Mobile Limited imeahidi kuboresha kazi za wanamuziki pamoja na asilimia ya malipo yanayotokana na milio na miito ya simu.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Freddie Manento katika mkutano na wanamuziki na wadau wa muziki uliofanyika kwenye hotel ya Serena.

Manento alisema hayo baada ya kuweka bayana mchakato mzima wa mfumo wa biashara ya muziki Tanzania katika mkutano uliohudhuria na wasanii zaidi ya 80 wa muziki wa aina tofauti ikiwa kama injili, bongo fleva, muziki wa dansi, taarab na reggae, hip hop na watayarishaji mbali mbali (producers).

Alisema kuwa kwa sasa Push Mobile inatoa wastani wa asilimia 20 mpaka 40 kwa mwanamuziki pamoja na wadau wao . Alisema kuwa kiwango hicho hutolewa baada ya wao kupokea kutoka kwa mitandao ya simu kati ya asilimia 35 mpaka 60.

“Lengo letu ni kuona wanamuziki wanafaidika na kazi zao hasa kupitia milio na miito ya simu, biashara ambayo kwa sasa imewaingizia kipato kikubwa wanamuziki baada ya kuanguka kwa soko la mauzo ya albamu e na kutopata kipato chochote kutoka kwenye redio na televisheni kama ilivyoelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia wakati anajibu hoja ya Mbunge wa Chadema, Zitto Kabwe,” alisema Manento.

Alisema kuwa asilimia ngapi wataongeza, itatokana na majadiliano na kampuni za mitandao ya simu na hata kama kampuni hizo zitakataa kuongeza ili kuwafaidisha wasanii, wao wataongeza tu.

Alifafanua kuwa kampuni yao imekuwa ikiingia gharama kubwa za kiuendeshaji katika kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata soko.

“Tunatumia si chini ya milioni 25 kwa mwezi kwa ajili ya kuandaa matangazo na kudhamini vipindi katika redio na televisheni kwa ajili ya kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata masoko, pia tunatumia zaidi ya million 7 kwa kazi ya kutengeneza nyimbo ili ziwezwe kuingizwa katika mifumo mbali mbali ya simu za mikononi,” alisema.

Kuhusiana na kuchelewa kwa malipo ya wanamuziki, Manento alisema kuwa tatizo hilo linatokana na ucheleweshwaji wa wadau husika kufanya malipo kwa wakati.

“Push imejitahidi kuondoa tatizo hilo kwa kuwalipa wanamuziki kwa fedha zake huku ikiendelea kudai kutoka kwa wadau husika ambao mara nyingine ukaa miezi sita bila kutulipa, ni changamoto kwetu, lakini tumejitahidi kufikia malengo na kutatua matatizo kwa wasanii, japo changamoto ni kubwa, nawaomba wanamuziki kuelewa tatizo hilo, ” alisema.

Akizungumza katika mkutano huo mtayarishaji maarufu wa muziki nchini, John Water Sharizo au Man Water aliipongeza Push Mobile kwa jitihada zake za kuinua kipato kwa wanamuziki kwani zamani walikuwa wananyonywa sana katika mauzo ya albamu.

Man Water alisema kuwa ni jukumu la Push Mobile ambayo inafanya kazi na wanamuziki wengi hapa nchini kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata faida na kazi zao kwani wao ndiyo wameingia mikataba na wanamuziki na wala siyo makampuni ya simu.

Alisema kuwa wanashukuru kwa kipato kilichopo kwani hapo awali walikuwa wanachapisha CD au kaseti 200 na kuuzwa mwaka mzima bila kupata mrahaba kinyume na sasa.

NGOMA MPYA YA TIP TOP CONNECTION - RIZIKI

PAH ONE NA CAMP MULLA WANAUFANANO

Japo si haki kuyalinganisha makundi haya kwa kuzingatia mafanikio na umaarufu kutokana na ukweli kwamba Camp Mulla wapo mbali zaidi na wanajulikana kimataifa kuliko Pah One, kuna mengi yakufanana katika makundi haya mawili. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa yote ni coincidence tu na hakuna lililoiga kundi jingine. Pah One wanawakilisha Tanzania na Camp Mulla wanawakilisha Kenya. 


Haya ni mambo kumi wanayofanana:

1. Makundi yote  yaliundwa miaka miwili ama mitatu iliyopita

2.Makundi yao yanaundwa na waimbaji/marapper wanne

PahOne – Aika, Ola, Nah Reel na Igwe

Camp Mulla - Taio Tripper, Shappa Man, Miss Karun, K'Cous , Japo yupo pia
Mykie Tuch ambaye ni CEO

Camp Mulla
3.Kila kundi lina wavulana watatu na msichana mmoja

PahOne – Aika

CampMulla -  Miss Karun

4. Kila kundi lina producer ambaye ni member pia na nyimbo zao hutengeneza wenyewe

PahOne – Nah Reel
Camp Mulla - K'Cous na Shappa Man


5. Wengi wana miaka chini ya 25

6. Wengi bado wanasoma

7. Karibu wote wanatokea kwenye familia bora
Pah One – Ola na Igwe wamesomea Afrika Kusini , Aika na Nah Reel wamesomea India

Camp Mulla – Mtandao mmoja uliwahi kuwaponda kuwa wanapendelewa kwakuwa wanatoka kwenye familia bora

Pah One
8. Muziki wanaofanya ni wa aina moja (Hip hop, dance na aina zingine za muziki wa kisasa)

9. Uvaaji wao unafanana sana

10. Wote wana akaunti maarufu ya mtandao wa muziki wa Reverbnation

KEKO KUKINUKISHA JIJINI MWANZA WEEKEND HII

 
 
Rapper wa kike toka nchini Uganda, Keko anatarajiwa kupiga show weekend hii jijini Mwanza.
 
Taarifa hiyo ameitoa mwenyewe kupitia Twitter account yake.

“TANZANIA ARE YOU READY!!! #KEKONIANS IN MWANZA #MAKEYOUDANCE COMING TO YOU THIS WEEKEND tell every & anyone KEKO Coming!!”

Hata hivyo mpaka sasa haijawa wazi ni nani anayempeleka jijini humo ama show itafanyika wapi kwakuwa hakuna matangazo yaliyotolewa.

THE MAKING OF BAADAE-OMMY DIMPOZ

KOFFI OLOMIDE ATUPWA JELA MIAKA MITATU


Stori kutoka Kinshasa Congo DRC zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina uzito ndani na nje ya Afrika, Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya star huyu wa rhumba mwenye miaka 56 apigwe nyundo hizo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake kwa jina la Diego Lubaki.
Nimemsikia mwandishi wa DW kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15 ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza kitatokea nini kwenye kesi yake August 16, 2012.Kabla ya kufikishwa Mahakamani Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi wa DW amesema ugomvi huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata hivyo meneja huyo aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga chini hilo ombi lake.
Baadhi ya wananchi waliotoa maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.
Kutokana na adhabu hiyo kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe.…