Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday 17 April 2013

MR. NICE AZALIWA UPYA!

Alikuwa moto kwelikweli at his times, Afrika Mashariki na Kati. Mr. Nice, mwimbaji wa ngoma kama ‘Kikulacho’ iliyomfanya avute mkwanja mrefu pengine kuliko msanii mwingine yeyote kwa wakati wote hapa Tanzania. Baada ya kupiga shows lukuki nje na ndani ya Tanzania Mr. Nice alianza kudrop taratibu na katika press conference yake leo hii alisema sababu yeye kushuka ilikuwa ni management yake.


Mr. Nice pia alikanusha kuwahi kuwa na bifu na Jose Chameleone wa Uganda. Zaidi ya hapo Mr. Nice alizungumzia kuhusu wimbo wa “Mac Muga” wa Ali Kiba kuwa haukuwa ukimuhusu yeye na maisha yake ya kimuziki, yaani kupanda na kuporomoka kwake! Mr. Nice alikana kuwa alikwenda Afrika Kusini, hali ya kimisha ikawa mbaya mpaka kurudishwa nyumbani Tanzania. Mr. Nice alikana kwenda Afrika Kusini na kusema kuwa Ali kIba hajawahi hata siku moja kusema kuwa ngoma hiyo inamuhusu yeye Mr. Nice!


The King is back. Mr. Nice amerudi upya katika game na this time amemshirikisha DNA toka Kenya, ngoma inaitwa ‘Tafuta’. Mr. Nice ame-sign label deal na Grandpa production ya Kenya na tarehe 26 April ataanza mfululizo wa kugonga shows hukohuko KE. 

Angalia video ya Mr. Nice feat. DNA:

BI. KIDUDE AFARIKI DUNIA!

Gwiji la muziki nchini Tanzania hususan taarab asilia, Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa kutoka katika familia yake zinasema Bi Kidude alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini imepoteza moja ya nguzo kubwa.

Pumzika kwa amani Fatuma Binti Baraka.