Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Sunday 3 February 2013

"MUHAMMAD ALI WA LEO AU KESHO"


“Bondia mkongwe duniani Muhammad Ali, 71,  atakufa wakati wowote ule”. Ni maneno ya kaka yake bondia huyo kutokana na hali aliyokuwa nayo. Inasemekana, Ali yu zofle hali, mahtuti kitandani! Rahman Ali ameongeza kuwa Ali haongei na hawezi kumtambua mtu yeyote. “Kama si miezi basi siku, Ali anaweza kututoka, tumwachie Mungu”, alisema Rahman.
Muhammad Ali
Rahman Ali
Muhammad Ali alipatikana  na ugonjwa wa Pakinson (kutetemeka mwili) mwaka 1984. Alionekana katika Olimpiki mwaka 1996 na mara ya mwisho 2012 huko London na alikuwa dhaifu mno kiasi cha kusaidiwa na mkewe kutembea. 
Rahman Ali anamtuhumu shemejie, mke wa Ali kwa kutoruhusu ndugu wa Ali kumtembelea. “Mara ya mwisho ilikuwa July ndipo niliongea na Ali, tena kupitia simu”, alifunguka Rahman.
Muhammad Ali na mkewe Lonnie
Mke wa Muhammad Ali, Lonnie amekataa kuzungumza lolote juu ya hali ya mumewe na tuhuma za Rahman.