Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday 7 January 2013

KIM NA KANYE WAKATAA OFA YA DOLA MILIONI TATU

Kim Kardashian na Boy friend wake Kanye west wanasemekana kukataa ofa ya dola milioni tatu (3) kwa picha za kipekee zitakazopigwa za mtoto wao ambae bado hajazaliwa kwa malengo ya kutabiri (prediction) kama mtoto huyo atafanana na nani? au atakuwa na labda pua ya Kanye West au Lips za Kim au vyovyote vile.
vyombo vingi vya habari vya magharibi vimekuwa vikiwania kupiga picha za kwanza kabisa pindi mtoto huyo atakapo zaliwa.



hata hivyo Joe Mullins ambae ni Forentic artist wa Marekani alizisoma picha za sasa za Kim na Kanye kisha kwa kutumia teknolojia ya sasa ya kompyuta akatabiri yafuatayo:-

uso wa mtoto wa kiume atakaezaliwa atarithi pua ya Kanye na shepu ya uso huku akiwa na mdomo kama wa mama yake ambae ni Kim.

MFANO WA PICHA YA MTOTO HUYO ANAETABIRIWA KUWA

RIO FERDINAND KUWA JAMES BOND WA KWANZA MWEUSI

Mchezaji wa soka wa klabu ya Manchester United ya Uingereza ameeleza kuwa atakapostaafu kucheza soka anatamani kwenda Hollywood kwaajili ya kufanya kazi ya film. angependa awe James Bond wa kwanza muafrika.