Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 23 August 2012

CHECK OUT RICK ROSS AKI-PEFORM KWENYE SUMMER JAM CONCERT HUKO NIGERIA

EXCLUSIVE: K LYNN IS PREGIOUS

Mama kijacho


List ya baby boom kwenye Miss Tanzania inataongeza siku si nyingi.
Baada ya Hoyce Temu, Nagris Mohammed, Miriam Gerald, Silvia Shally na Nancy Sumari ambao waliwahi kuwa mamiss Tezee kumuongezea Uncle Lundenga cheo cha U-uncle baada ya kujaliwa watoto,  latest news ni kwamba Jacquline Ntuyabaliwe better known as K Lynn naye yuko mbioni kuongeza mjomba mwingine coz she's now eating for two.



Habari za uhakiaka zinadai kuwa jamaa mwenye makampuni MEEENGI hapa nchini ndiye aliefanikisha zoezi hilo.

P SQUARE NEW AUDIO - ALINGO

MB DOGG KWENYE MOVIE


Filamu kali na ya kusisimua ya Nankonda wa Mikindani inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni ndio itakayokuwa filamu ya kwanza kumtambulisha msanii wa  Bongo fleva  kwa jina la Mbwana Mohamed  aka ‘Mb Dogg’ kuingia katika tasnia ya filamu.
Filamu hiyo ambayo Mb Dogg amacheza kama mhusika mkuu imetayarishwa na Dr. Cool Production company.
 “Uwezo alionyesha Mb Dogg ni wa hali ya juu sana, utafikiri alikuwepo katika tasnia ya uigizaji kwa miaka mingi , msanii amebeba uhusika kulingana na hadithi yenyewe nasema ni msanii anayejua kuigiza na hilo mtalismtalishuhudia katika filamu hiyo,” said Mzee Korongo.

NYUMBA MPYA YA CEO WA CASH MONEY

Ronald Williams Aka Slim ambaye ndio C.E.O Wa Cash Money ndiye amenunua nyumba ya thamani ya Dollar zaki Marekani Milliom $ 7.15. Ni Nyumba yenye vyumba 9 vya kulala ,Mabafu 12. 
Unuunnuzi wa nyumba hii umekuwa wa siri sana kitu ambacho ni tafauti na wasanii wa kundi hilio la Cash Money huwa wanapenda kutangaza mambo yao yote ya thamani. Ronald ni kaka wa Bryan 'Birdman' Williams na ni mmoja wa wadau matajiri sana kwenye mziki Marekani mwenye Thamani ya Dollar za Kimarekani Million $100



CHECK THIS OUT...IS KANYE A BODYGUARD TO KIM?








 
 
 
 
 


 
 











BREAKING NEWS: KALALA JUNIOR AREJEA TWANGA PEPETA

Kalala mwenye shades akiwa na wasanii wengine wa Twanga mapema leo

Chezea Asha Baraka wewe.
Baada ya kujeruhiwa na wamiliki wa Mashujaa Band kwa kuwachukua wasanii wake nguli akiwamo Charlz Baba, round hii Asha ambaye ni manager wa Twanga Pepeta amefanya vitu vyake baada ya leo hii kumrudisha kundini Kalala Junior ambaye miezi miwili iliyopita aliikacha band ya Mapacha Watatu alikokuwa akipiga mzigo.
Ikikumbukwa vizuri miaka michache iliyopita Kalala alijitoa Twanga na kwenda kujiunga na Mapacha Watu alikokuwa akishirikiana na kina Jose Mara na Khalid Chokoraa. 
Unaambiwa katiaka hali ya kuonyesha karudi nyumbani kwa hasira, tayari Kalala amesha-record nyimbo mbili ziitwazo  "Nyumbani ni Nyumbani" na "Ushirika ni Sawa na Koti Likikubana Livue".


SCOPION GIRL - WATUACHE VIDEO

MAISHA PLUS IZ BACK



Maisha Plus is back na shughuli ya kusaka washiriki wa kuingia kijijini   mwezi October utaanza rasmi siku ya Jumatatu ijayo kwa ajil.
Tofauti na usaili wa mashindano yaliyopita, vijana hao 26 watatafutwa katika vijiji ambavyo Mama Shujaa wa chakula wapatao 15 walipatikana kutokana na mchakato uliofanywa na shirika la chakula na kilimo la Uingereza la Oxfam ambalo msimu huu litashirikiana na waratibu wa shindano hilo.
“Vijana wa Maisha Plus wataingia kijijini, watakwenda kuchanganyika na hao kinamama, watakaa kwa siku tatu jumla kwa maana ya kwamba watakaa siku 12, 13 na siku 14. Katika hizi siku tatu vijana watakapochanganyika na hawa akinamama mle ndani tutatengeneza makundi ambapo kila mama mmoja mzalishaji wa chakula atakuwa na timu ya vijana tuseme watatu, wanne, sita kulingana na idadi ya washiriki wa Maisha Plus ambayo mwaka huu imeongezeka kutoka 18 hadi 26", Masoud Kipanya ambaye ndiye mratibu wa shindano hilo.
Mshindi wa mwaka huu atakamata kitika cha shilingi milioni 20.

PREZZO IN NAIJA - ATANGAZA NIA YAKE YA KUTAKA KUMUOA GOLDIE


The Big Brother Africa star game second runner up Prezzo anataka kumuoa Goldie kama atalikubali ombi lake..
Mkenya huyu mwenye miaka 32 ambaye kwa sasa yuko Nigeria, amesema safari yake ya kutoka Kenya 'haikuwa ya kwenda kucheza nchini humo' bali ameenda ku-express hisia zake za mapenzi kwa Goldie.
Prezzo, ambaye aliwaomba Wanigeria msamaha kwa jinsi alivyom-treat Goldie kwenye mjengo wa BBA, amesema anatangaza nia yake hadharani ya kutaka kumuoa Goldie kwani hata kukutana kwao kulikuwa hadharani akiongeza kuwa yuko tayari kwa lolote ambalo litamfanya kumfanye bibie huyu kuwa Mrs Prezzo.
"Sikuwa na uwezo wa kuonyesha feelings zangu zote kwa Goldie pindi tukiwa kwenye jumba la BBA kutokana na paranoia lakini kwa sasa niko tayari kupambana ili kuishinda zawadi hii itakayo nifanya niwe mshindi halisi....
Will Goldie say YES I DO kwa Prezzo...., lets wait.

THE RETURN OF J LO YA SINTA TAYARI

Cover ya movie ya Sinta


Mwezi ujao kuna movie mpya inaingia sokoni. Inaitwa The Return of JLO.

Kwenye filamu hiyo Sintah ndo main character ambapo wengine watakaonekana ni  Chalz Baba, Beny Kinyaiya, Monalisa, Nyoshi El-sadat na wengine.

Filamu hiyo imeandikwa na kuongozwa na Selles Mapunda wa Steps Entertainment.

TUKINAO NDIYE BIBI BOMBA 2012

Fainali ya lile shindano la kumsaka BIBI BOMBA lililokuwa likirushwa na Clouds TV ilifanyika jana mjengoni ambapo bibi Veronica Mpangala aka Tukinao aliibuka kidedea na kuondoka na zawadi ya shilingi milioni tano toka kwa wadhamini wa shindano hilo.

Bibi Veronica akiwashukuru wapiga kura wake kwa kumpigia kura hadi kuibuka kidedea

 
Anold (kulia) toka Zantel akimkabidhi bibi bomba mfano wa check.Katikati ni host wa show hiyo Babuu wa Kitaa.
Anna Said mshindi wa pili
Nasra Mohamed mshindi wa tatu

Finalists wa shindano hilo
Ruge akiwapongeza bibi bomba