Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 16 May 2013

D' BANJ ALA SAHANI MOJA NA BARNABA BOY

Wakati wasanii wa Kibongo wakihaha kutafuta michongo mbalimbali ya kuwaingiza mkwanja ikiwemo kupata haki sahihi ya umiliki wa ringtones zao na zaidi kupata mashavu ya kuwa mabalozi wa makampuni mbalimbali, huko kwa wenzetu hasa West Africa wameshapiga hatua kubwa sana katika hili.

Achilia mbali tuzo lukuki na hits anazozidondosha siku baada ya siku, neema zinaonekana bado kumdondokea artiste huyu kwani leo hii KokoMaster a.k.a D’ Banj alisaini mkataba wa kuwa balozi wa benki moja huko Naija iitwayo Bank of Industry.
Ms Evelyn Oputu, Managing Director & Chief Executive Officer of Bank of Industry na balozi D' Banj


 
Hapa Tanzania hii imekuwa hatua mpya sasa hasa kwa upande wa mabenki kuwachagua wasanii wazawa kuwa mabalozi wake na mfano hai tu ambao kidogo unaendaana na huo wa msanii kuwa balozi ni wa Barbana Boy kufanya kazi na benki ya Barclays Tanzania (japo Barnabas si balozi wa benki hiyo) lakini cha msingi ni lile dili tu kati yake na benki hiyo ambapo Barnabas ataingiza zaidi ya dola za Kimarekani 20,000/=kwa kuimba wimbo juu ya wanawake wa Kitanzania.