Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday 26 August 2013

SHOW YA UCHI YA MILEY CYPRUS KATIKA VMA 2013

Picha tofauti za Miley Cyprus na Robbin Thicke katika jukwaa la Video Music Awards (VMA2013). Chini kulia ni familia ya Will Smith wakishangaa wasiamini kinachotokea jukwaani!

Friday 23 August 2013

SKETI YAMVUKA TONI BRAXTON STEJINI!

Mwanzomi mwa wiki hii huko New Jersey, mama wa watoto wawili, mwanamuziki Toni Braxton aliwapa mashabiki wake zaidi ya kile walichokilipia kwaajili ya show hiyo. Wakati akiwa stejini akipiga show hiyo Toni Braxton, 42, alishangaa akiona sketi yake nyepesi ya metallic akimvuka na kuacha makalio yake wazi!




Kwa bahati mbaya Toni Braxton hakugundua kuwa sketi yake imemvuka kwani aligeuka na kuwapa mashabiki mgongo huku akitingisha makalio yake kwa mbwembwe asijue kinachoendelea kumbe ndio anawamwagia utamu huku mashabiki wakilipuka kwa shangwe la hatari!



Toni Braxton aliendelea na show mpaka jamaa mmoja alipokwea stejini na kumfunika kwa koti la suti yake.



Thursday 22 August 2013

DIAMOND KULA MKWANJA MREFU KWA KUFANYA COLLABO KENYA

Mshindi wa tuzo ya mwimbaji bora wa Gospel nchini Kenya, Willy Paul ametangaza kupiga kolabo na msanii mwenye kukamata headlines kila uchao Bongo na nje ya Tanzania, Diamond Platinumz! Willy alikutana na Diamond katika concert moja iliyohappen huko Nairobi Ijumaa iliyopita.

"Diamond alivutiwa sana na kazi zangu kama mimi kwa kazi zake. Nafahamu anachaji pesa so nitamsikiliza anahitaji kiasi gani na nipo radhi kumpa mkwanja autakao". 


.


BRANDY AGOMA KUPIGIA SHOW VITI!

Mwanadada Brandy hakuwa na siku nzuri siku ya Jumamosi iliyopita baada ya kupiga show kwa watu 40 tu kati ya mashabiki 90,000 waliotakiwa kuingia katika show hiyo. Hii ilitokea hapo kwa Madiba, katika uwanja wa FNB stadium, Afrika Kusini katika siku maalum ya 'Mandela Sports and Culture day'. 

Tatizo lilitokea ni kuwa mapromota wa event hiyo hawakuwataarifu watu waliohudhuria shughuli hizo kwani baada ya shamrashamra za hapa na pale raia wakaondoka wakijua shughuli imeisha kumbe Brandy aliwekwa kama 'surprise artist '. Ndipo hapo sasa mwanadada huyo alipopanda stejini na kuwaimbia watu wasiopungua 40 tu huku viti zaidi ya 80,000 vikiwa tupu! Baada ya kupafomu ngoma mbili tu Brandy aliacha steji na kusepa zake!


STAR WA PRISON BREAK AJITANGAZA NI SHOGA!

Starring wa tamthiliya ya Prison Break, Wentworth Miller a.k.a Michael Scofield ametangaza jana Jumatano kuwa yeye ni shoga. Amefanya uamuzi huu baada ya kukataa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za jumuiya ya wanafilamu katika mchakato wa kukataa au kupinga 'ushoga' nchinu Urusi.


Baada ya Michael Scofield kupokea mwaliko huo uliopewa jina la St. Petersburg International Film Festival, alisema, "Mimi kama shoga ni lazima nikatae". Scofield aliendelea kusema, "Nachukizwa na vile jinsi mashoga na wasagaji wanavyochukuliwa na serikali ya Urusi. Kwahivyo siwezi kushiriki katika kampeni hii ambapo watu kama mimi hawapewi haki zao za msingi"


Tuesday 20 August 2013

BOBI WINE AMCHANA BEBE COOL!


Ni muda sasa umepita tangu bifu la Bobi Wine na Bebe Cool lianze na sio kwamba linaelekea kufifia au kufa, la, bado mafahali hawa wawili hawaivi chungu kimoja! Na juzi tu Bobi Wine alikuwa na haya kumwambia Bebe Cool.
 

"Sina tatizo lolote na Bebe Cool lakini ana matatizo na yeye mwenyewe, ni kama vile watoto wadogo wakati mnakua. Wengine hukua na kupevuka haraka na wengine hubaki nyuma kama yeye ila sitaki anirudishe nyuma. Ni kama vile niliponunua ndege yangu, yeye hupenda kuzungumzia vitu vyangu kwa vile nam-inspire, inafurahisha sana"







 

Saturday 17 August 2013

CHRIS BROWN ATUPWA JELA

Itabidi abadilishe ratiba yake upya kwa masaa 1,000 toka sasa baada ya mahakama ya huko Los Angeles kumhukumu Chris Brown kwa kufanya kazi za jamii. Hukumu hii inakuja baada ya Chris Brown kuonekana aliwasilisha ripoti ya uongo inayoonyehsa kuwa alitumikia kiukamilifu adhabu ya aliyopewa awali ya kuitimikia jamii kwa siku 180.

Kosa hili la kuwakilisha ripoti feki inatokana na adhabu aliyopewa baada ya kukutwa hatia ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna.


DORICE MOLLEL NDIYE RED'S MISS ILALA 2013

Kanda ya Ilala usiku wa kuamkia leo ilimtoa mlibwende atakaeiwakilisha kanda hiyo katika Miss Tanzania mwaka huu. Aliyekuwa Miss Ilala Dorice Mollel jana alivikwa taji la Red's Miss Ilala 2013, na kujichukulia kitita cha 1.5 milioni. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Alice Isaac (1 milioni) na wa tatu ni Clara Bayo (laki 7). 


Thursday 15 August 2013

RIHANNA TENA

Mwana Muziki Machachari Rihanna haachi vituko kila kukicha na hiki ndicho kituko kipya










REDD'S MISS ILALA NI IJUMAA HII

Shindano la kumsaka mlimbwende wa Ilala litafanyika siku ya ijumaa tarehe 16/08/03 kuanzia saa 2 za usiku katika ukumbi Mpya na wa kisasa katika jengo la GOLDEN TOWER
Katika kuelekea kilele cha shindano hilo jana usiku kulifanyika shindano la vipaji katika ukumbi wa city sport longe ambapo wasichana watano kati ya 10 walioshiriki shindano hilo walifanikiwa kutinga  fainali ambapo fainali hzo zitaendana na sambamba na kumpata Redd;s Miss Ilala 2013.
Cheki picha mbali mbali za tukio hilo.









JAY Z NA DIDDY WAMCHEKA KENDRICK LAMAR

Fasta baada ya kujitangazia Ufalme wa jiji la New York, The hot Hip Hop star Kendrick Lamar amepata majibu. Majibu yanatoka kwa legends ya game ya Hip Hop duniani, Jay Z na Sean Comb 'Diddy' kwa kusema kuwa dogo huyu ana utani sana! Kwa upande mwingine Jay na Diddy wameichukulia kauli hii kama kutafuta kiki tu ya kimuziki! 


Friday 9 August 2013

MAJERUHI WA TINDIKALI ZANZIBAR HAWA HAPA

RAISI AWAFARIJI MAJERUHI AGA KHAN HOSPITAL
                       Kabla ya Tukio

                            Baada ya kumwagiwa Kitu kinacho zaniwa ni                 maji maji ya tindi kali                     
    Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dr J.M.Kikwete
   akitoka Hospita AGA KHAN kuwajulia hali