Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 22 August 2013

BRANDY AGOMA KUPIGIA SHOW VITI!

Mwanadada Brandy hakuwa na siku nzuri siku ya Jumamosi iliyopita baada ya kupiga show kwa watu 40 tu kati ya mashabiki 90,000 waliotakiwa kuingia katika show hiyo. Hii ilitokea hapo kwa Madiba, katika uwanja wa FNB stadium, Afrika Kusini katika siku maalum ya 'Mandela Sports and Culture day'. 

Tatizo lilitokea ni kuwa mapromota wa event hiyo hawakuwataarifu watu waliohudhuria shughuli hizo kwani baada ya shamrashamra za hapa na pale raia wakaondoka wakijua shughuli imeisha kumbe Brandy aliwekwa kama 'surprise artist '. Ndipo hapo sasa mwanadada huyo alipopanda stejini na kuwaimbia watu wasiopungua 40 tu huku viti zaidi ya 80,000 vikiwa tupu! Baada ya kupafomu ngoma mbili tu Brandy aliacha steji na kusepa zake!


No comments:

Post a Comment