Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday 6 May 2013

PAUL WA P-SQUARE AKATAA MTOTO WA PILI!

Katika kipindi kisichopungua mwezi mmoja, Paul Okoye amepata mtoto wa pili, tarehe 11 April demu wake wa siku nyingi, Anita alijifungua mtoto wa kiume, Andre Paul Okoye. Na sasa kuna taarifa zinasema kuwa demu wake mwingine, Elshama Benson Igbanoi, 19, amejifungua mtoto wa kiume huko Queen Charlotte and Chelsea Hospital, London na kupewa jina la Michelle Paul Okoye.
Michelle Paul Okoye
Chakushangaza Paul amemkataa mtoto huyo huku akiahidi kutua London ili kufanya DNA test kabla ya kukubali wajibu wake kwa mtoto kama baba. Baba wa binti huyo, Mzee Igbanoi amesema kuwa ameshamtumia e-mails za kutosha Paul toka binti yake akiwa mjamzito mpaka anajifungua lakini Paul hajajibu lolote.

Kuona hivyo Familia ya Mzee Igbanoi imeshafanya utaratibu wa kuwasiliana na Baba na Shangazi wa Paul huku akikazia kuwa binti yake hajawahi kuwa na mwanaume mwingine isipokuwa msanii huyo Paul Okoye ambaye ndiye alimtoa bikira Elshama akiwa na umri wa miaka 17.

Elshama
Mpaka sasa bado gharama za hospitali zinazozidi pauni 5,000 hazijalipwa na Elshama. Inasemekana kuwa Elshama ni rafiki pia wa Anita, msichana aliyemzalia huyuhuyu Paul Okoye mtoto wa kwanza tarehe 11 mwezi huu!

Paul Okoye na mtoto wake wa kwanza, Andre Okoye