Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday 26 July 2013

BUSTA RHYMES KUPAFOM KENYA

Sasa rasmi kuwa busta Rhymes a.k.a Trevor Taheim Smith Jr atatua Kenya kwa ajili ya kazi moja tu, nayo ni kuwarusha maraia wote wa 254. Hiyo itakuwa mwezi September, 2013. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Busta kuja Kenya na anatarajiwa kupagawawisha crowd litakalotokea kwa ngoma zake zilizotamba kama 'Twerk It' na Nicki Minaj, 'I Got What You Want' na Mariah Carrey, 'Look at Me Now' akiwa na Chris Brown, 'Touch It with the whole world' na ngoma nyingine lukuki!




Thursday 25 July 2013

GENEVIVIE ANA MIAKA 10 HAJA-DO!

Hii imechukuliwa kama gia ama kick ya kumlegeza bwana wake ili aharakishe ndoa yao kwa mwanamama mahiri katika tasnia ya uguzaji, Genevivie Nnaji kusema kuutangazia umma kuwa, ana miaka kumi toka alipofanya ngono kwa mara mwisho. 



Hivi ndivyo Nnaji anavyofunguka,

      "Nimekuwa single na mpweke kwa muda mrefu.                         Hata nilipokuwa na D'banj, mahusiano yetu                               yalikuwa ya muda mfupi sana kinyume na matarajio                 yangu. Namshukuru Mungu sasahivi nimempata                       mwanaume ambaye nitamaliza naye maisha yangu yote"

Wednesday 24 July 2013

NYAKATI MBILI MBAYA ZA BEYONCE!

Hii ilikuwa ni tour yake iitwayo 'B-Day tour' akiperform 'Ring the Alarm'. Hapa alidondoka mzima mzima wakati akipanda ngazi za steji.


Katikati ya show yake ya mwezi March mwaka huu, Beyonce alimpa microphone shabiki wake aliyekuwa na midadi kwelikweli, ili nae aimbe kidogo japo mistari miwili mitatu. Kumbe jamaa hajui lolote. Shabiki huyo,  Princess Eugenie alipopewa mic aligeuka bubu ghafla. Whoops!


WASANII WATANO WASIOJUA KUIMBA JAPO MASHABIKI WANAWAKUBALI!

1.KEYSHIA COLE
Inatakiwa atafutwe mtu amwambie binti huyu wa Frankie kuwa sauti yake haijakaa sawa. Ni lazima atafute mwalimu wa sauti ili amuweke sawa.


2.ALICIA KEYS
Baada ya kuzaa, Alicia amerudi tena kuwa mzuri ajabu kimuonekano. Lakini kiumbaji hasa vocally, wataalam wa mziki wanasema ameshuka sana. Na hii ni baada ya kuambatana na mumewe Swizz Beatz. Sauti yake haijarudi na kuwa tamu tena.

3.JUSTIN BIEBER
Ana uwezo mzuri wa kulimiliki jukwaa lakini linapokuja suala la sauti, Bieber hamgusi Usher hata Maxwell. Kwa mwendo huu miaka kumi toka sasa anaweza kuwa amesahaulika.


4. MICHELLE WILLIAMS
Michelle anaboa sana. Sauti yake bado haijawa ile ya kuweza kumuweka katika list ya waimbaji bora USA kutokana na vile ana pata shida sana kufikia nota za juu katika uimbaji wake. Alikuwa memba wa Destiny child. Pengine hii ndio sababu iliyomfanya asionekana kung'aa katika kundi hilo lililovunjika na hata kupotea kabisa tofauti na Beyonce na Kelly Rowland. 


5. ROBIN THICKE
Robin anaonekana mlazimishaji kwelikweli. Anataka kwenda high notes lakini hafiki inavyotakiwa kimuziki. Tafura performace yake ya BET 2013.


Thursday 18 July 2013

NUKUU YA LEO

DIAMOND ASHIKA NAMBA MOJA AFRIKA MASHARIKI!

Kubali au kataa, mpende au mchukie lakini ukweli utabaki palepale kuwa kwasasa msanii toka Tanzania, Diamond Platnumz a.k.a Naseeb Abdul ndio mwenye nguvu kubwa zaidi katika majukwaa yote ya Afrika Mashariki.



Kwa mujibu wa website moja huko Kenya anayemfuata kwa ni nguli Dk. Jose Chameleone ambaye kwa kipindi kirefu sana ameweza kukusanya raia wengi popote pale anapopiga show hasa East Africa. Achana na Chameleone, Diamond hivi sasa ameonekana kung'arisha zaidi huku makampuni makubwa hasa ya Kitanzania kila leo yakibisha hodi nyumbani kwa Diamond ili kuingia naye mikataba (endorsements).

Moja kati ya vipimo sahihi vya Diamond kuwa juu kwasasa ni ile show ya Congo iliyosababisha foleni ambayo haijawahi tokea huko Congo kutokana na umati uliopitiliza kumwagika barabarani! Pia kuna hii tour ya Burundi. Nyomi la hatari lilimwagika kupita mategeo ya waandaaji.



MISS KERI AMUOMBA MSAMAHA BEYONCE

Kutoka kwa producer mkali huko USA, Timberland, amesema kuwa 'Energy' hitmaker, Miss Keri yupo studio akitengeza ngoma kali iitwayo'Sorry' mahsusi kwaajili ya kumuomba radhi King Bey. Timberland amebreak the news kuwa kutokana na kutapakaa uvumi kuwa Miss Keri alimdiss Jay Z's wify basi sasa huu ni wakati muafaka wa kuanika kila kitu hadharani ili fans wa Keri na Bey wafahamu nini hasa kilitokea na yote hayo Keri ameelezea katika ngoma hiyo mpya ya 'Sorry'.

Just stay tuned kwasababu ngoma hii utaipata hapahapa!



Saturday 6 July 2013

FEZA KESSY AMWAGA MITUSI KWA KISWAHILI MJENGONI

Mshiriki wa Tanzania katika jumba la big brother amejitengenezea mazingira ya kutoka mapema kwenye game baada ya kuanza kuonyesha tabia yake halisi kama ni mgomvi na anaetumia lugha chafu bila ya aibu.
ikiwa mida hii party inaendelea kulikua na  sitofahamu ya Oneal na Feza wakizozana huku Feza akimtuhumu Oneal ukaribu wak na Pokello kitu kinacho mpa mashaka kwani Feza na Oneal ni wapenzi ndani ya mjengo huo sasa ule wasi wasi wa Mapenzi umemuingia Feza.
Baada ya Feza kuingia kweny paty alienda moja kwa moja kwa mwakilishi wa Kenya Annabel na kumwambia kwamba Pokelo ni Mngese na lile tusi jingine  Kuuuu  m*****k***Feza alitamka matusi hayo katika lugha ya Kiswahili nazani alitaka Pokelo asielewe hayo Matusi.
je Feza hapo anajiweka katika nafasi gani ndani ya jumba hilo

      Feza
                             Pokello
    Feza & Oneal

  Feza & Oneal  siku ya harusi ndani ya Mjengo wa BBA

Wednesday 3 July 2013

NANDO KUTIMULIWA BBA

Mwakilishi wa Tanzania Nando  katika jumba la Big brother huenda akatimuliwa.
kwa mujibu wa big ambae alimuita Nando kumpa habari hyo, na kisa chenyewe ni Nando baada ya kuingia na Kisu katika party ambayo big huwaandalia kila siku ya jumamosi.
Big alimuita Nando katika Diary room nakumuonyesha clps ya video ambayo ilionyesha Nando ameshika kisu na alipo ulizwa ni kwa nini alikua na kisu wakati ni hatari kwa usalama wake na washiriki wenzake Nando alijibu alijisahau alipo maliza shughuli ya kutumia kisu kukiacha na badala yake alikiweka mfukoni lakini hakua na nia ya kumzuru mtu Big alimwambia akawaeleze washiriki wenzake kwa nini aliingia na kisu na alifanya hivyo kwa kuwaeleza ni kawaida yake hata akiwa nyumbani anapenda kucheza na kisu na hapo alijisahau lakini hakuwa na nia ya kumzuru mtu na akaomba msamaha 
lakini washakunaku kwenye jumba hilo wanaona ni kama wivu wa mapenzi ulimpata baada yeye na Sulu wote wakiwa wanachezewa akili na binti mtata Selly Big amempa onyo la Mwisho Nando na akifanya kosa jingine atafukuzwa kwenye jumba hilo.

 Nando
  Fatima ,Nando na IK

Tuesday 2 July 2013

CHRIS BROWN, RIHANNA NA DRAKE WATAKATA BET AWARDS 2013

Juzi Jumapili ilifanyika ile show the best kwa watu weusi huko United States of America maarufu kama BET awards. Awards hizi kwa 2013 zilitolewa katika ukumbi wa Nokia Theatre, Los Angeles na baadhi ya wasanii waliofanya vizuri ni pamoja na Chriss Brown, Rihanna, Drake na wengine kibao. 
Nick Minaj
Ice Prince
Kwa Africa, rapper Ice Prince toka Nigeria aliwagalagaza big names kama 2face Idibia, Toya Delazy (South Africa), Donald (South Africa), R2Bees (Ghana), Weasal na Radio (Uganda). List nzima ya washindi na tuzo walizokamata ni kama ifuatavyo;-


Best Female R&B/Pop Artist: Rihanna

Best Male R&B/Pop Artist: Chris Brown

Best Group: Macklemore and Ryan Lewis

Best Collaboration: A$AP Rocky (featuring Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar) – F***in’ Problems

Best Male Hip Hop Artist: Kendrick Lamar

Best Female Hip Hop Artist: Nicki Minaj

Video Of The Year: Drake – Started From the Bottom

Video Director of the Year: Benny Boom

Best New Artist: Kendrick Lamar

Best Gospel Artist: Mary Mary

Best Actress: Kerry Washington

Best Actor: Jamie Foxx

YoungStars Award: Gabrielle Douglas

Best Movie: Think Like a Man

Subway Sportswoman of the Year: Gabrielle Douglas

Subway Sportsman of the Year: LeBron James

Coca-Cola Viewers’ Choice Award: Drake – Started From the Bottom

Centric Award: Tamar Braxton – Love and War

Best International Act: Africa  – Ice Prince (Nigeria)

Humanitarian Award: Dwyane Wade

Lifetime Achievement Award: Charlie Wilson

FANdemonium Award: Chris Brown