Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Sunday 17 February 2013

MARY J. BLIDGE AFILISIKA, MADENI KIBAO!


Kama unafikiri matatizo ya kufilisika kwa The Queen of Hiphop and Soul, Mary J. Blidge yamekwisha basi si kweli, mwanamama huyo ameingia katika msala mwingine wa kutakiwa kulipa kodi ya dola 900,000 huko New Jersey!

Hii ni baada ya mwanzoni mwa wiki iliyopita kushtakiwa kwa kuchelewa kulipa mkopo wa benki, dola 500,000. Ni mwaka uliopita tu Blidge alishtakiwa kwa kwa kutolipa mkopo wa benki wa dola milioni 2.2, na kabla ya hapo kituo chake kilishtakiwa pia kwa kosa hilohilo la kutolipa deni la dola 250,000.

Mary J. Blidge


RIHANNA AJA NA MAVAZI YAKE!

Baada ya kujijengea jina kubwa katika ulimwengu wa muziki duniani sasa Rihanna anaenda extra mile kwa kuingia rasmi katika tasnia ya ubunifu wa mavazi! Kwa mara ya kwanza this Barbadian singer aliingiza style mpya ya mavazi katika wiki ya mavazi huko London, London Fashion Week, jana Jumamosi!



The Stay singer alipata mapokezi mazuri toka kwa mashabiki na hata watu mashuhuri akiwemo Toni Jones aliye-comment kuwa mavazi hayo ‘yanavutia’ na ‘kuvalika’ pia!

Mavazi ya Rihanna yamelenga zaidi kuvaliwa na vijana na hasa ameanza na wa kike!











Angalia kipande kidogo cha video ya show hiyo: