Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday 16 March 2013

ALINGO Vs AZONTO

Kumeibuka ghasia na kutupiana kwa maneno katika mitandao ya jamii baina ya Wanigeria na Waghana kuhusiana na styles hizi mbili za Alingo na Azonto. Na sokomoko hili limekuja hasa baada ya artiste wa dancehall toka Ghana, Samini kutoa ngoma kwa kutumia biti ya Alingo kuwadis P-Squae kwa kukopi dance ya Azonto na kuitumia katika Alingo!

 Wewe unafikiri style ipi ya ku-dance ni kali kati ya ile ya Azonto na Alingo? Na je, ni kweli styles hizi zinafanana?















































LIL WAYNE BADO YUPO HOI HOSPITALI!

Young Money Cash Money brother, Lil Wayne alikimbizwa hospitali hivi majuzi baada ya kuzidiwa. Hali yake ilikuwa mbaya sana kiasi cha kukutwa akiwa sakafuni chumbani kwake hajitambui. Mpaka sasa hali ya Wayne si nzuri sana licha ya ku-tweet kuwa yupo poa!


Ndugu, jamaa, marafiki na rap artistes kadhaa walimiminika hospitalini siku ya Jumatano kumjulia hali Wayne. Hali hii ya Lil Wayne inatokana na ubwiaji unga aina ya codeine uliopitiliza. Inasemekana madaktari walikuta kiasi kikubwa cha madawa hayo mwilini mwa Wayne hivyo kupelekea madaktari kuamua kuusafisha mwili wa Wayne mara tatu.

Pamoja na hayo yote jana Ijumaa Lil wayne aliibuka na ku-tweet kuwa yupo fresh na kuwashukuru fans wake kwa sala zao na upendo kwake!