Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday 18 July 2012

FINA MANGO ATUA MAGIC FM


Baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kusikika redioni mashabiki wa Fina Mango wana uhakika wa kuanza kuisikia tena sauti yake tamu.

Mtangazaji huyo wa zamani wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, hatimaye  amehamia Magic FM.

Akiwa Magic FM, Fina Mango atakuwa akiendesha kipindi cha 'Mkutano' ambacho kitakuwa kikisikika kila  Jumamosi kuanzia saa 9.00 alasiri – 12 jioni.

Kipindi hicho kiitwacho ‘Makutano’ kitaruka kwa mara ya kwanza tarehe 4 mwezi ujao (August).
“My first radio crush is making a comeback…all the best @Fina_Mango cant wait to hear you again on air,” aliandika shabiki wake wa zamani aitwaye Lijocha.
Apparently, Fina Mango atafanya kipindi hicho kwa makubaliano maalum na sio kuajiriwa kwakuwa tayari ana kampuni yake iitwayo 1Plus Communications.