Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday 10 June 2013

RIHANNA AVUNJA REKODI UFARANSA

Haijawahi kutokea! Katika umri wa miaka 25 tu, Rihanna ameweza kuweka historia kwa kuujaza uwanja wa kandanda wa Stade De France alipogonga show yake ya wazi Week-end hii. Ni Lady Gaga pekee ndio aliyekuwa ameishikilia rekodi hiyo kwa kuutitirisha uwanja huo akiwa na umri mdogo, miaka 26 lakini Rihanna amemfunika vibaya Lady Gaga huku Rihanna akiwa ana miaka 25 tu.


Mmoja kati ya fans wake ali-tweet hivi baada ya show hiyo:
"Rihanna is also the youngest person to ever headline Stade De France"




CHRIS BROWN MAHAKAMANI LEO

The bad boy Chris Brown anatarajiwa kukutana uso kwa uso na pilato leo hii mezani kukiwa na mashtaka yanayomkabili kwamba hakukamilisha muda rasmi aliotakiwa kuitumikia jamii (community service), ikiwa kama adhabu baada ya kukutwa na hatia ya kumchapa makonde aliyekuwa girlfriend wake, Rihanna, mwaka 2009. Chriss Brown alitakiwa aitumikie jamii kwa siku 180 na April mwaka huu alikuwa mahakama lakini pilato aliihairisha kesi hiyo baada ya kukosa baadhi ya taarifa muhimu.


Chris Brown yupo mbioni kutoa albam yake ya 6 iitwayo "X", tarehe 16, July akiwashirikisha Kendrick Lamar, Nicki Minaj, Wiz Khalifa na Jennifer Lopez na tayari ameshatanguliza ngoma ya 'Fine China" ambayo ipo namba 31 katika Billboard Hot 100 chart. 


KANYE WEST ASHEREHEKEA BIRTHDAY BILA KIM KARDASHIAN

Kanye West ametimiza miaka 36 na kuangusha bonge la party la kimya kimya. Party hili liliwahusisha watu wake karibu tu wakiwemo Beyonce na Jay Z. Nas pia alikuwepo mjengoni. Ila kilichowashangaza watu wengi ni kutoonekana kwa mama kijacho wake, Kim Kardashin. 


Lakini wataalam wa mambo wanasema kuwa Kim K alishindwa kupaa mpaka New York kwavile yupo katika nyakati za majeruhi akikaribia kabisa siku zake za kumleta duniani mtoto wake wa kwanza ambaye tayari madaktari wameshasema kuwa atakuwa mwenye jinsia ya kike!