Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday 19 March 2013

OBAMA AFANANISHWA NA SHETANI!

Kupitia kituo cha television cha History Channel, tamthiliya ya "The Bible" inayoonyeshwa kupitia channel hiyo imekuwa gumzo kutokana na 'shetani' anayeonekana katika movie hiyo kufanana na rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama. 
 
Tamthiliya hii ya kidini imetengenezwa na Mark Burnett na kuchezwa na Mehdi Ouzaani imevuta hisia za watazamaji wengi na kwa kuonekana kwake siku ya Jumatano iliyopita imeweza kutazamwa na watazamaji milioni 13.1

















MWONEKANO WA AMBER ROSE BAADA YA KUJIFUNGUA!

Kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja Amber Rose alikuwa very busy akimlea mtoto wake Sebastian. Sasa A.Rose anaweza hata kuchat katika mitandao ya kijamii na fans wake, kushare pics na hata kutoka nje for shopping.




Amber rose na mama yake wakifanya shopping


D' BANJ AJA NA DOCUMENTARY!

From Lagos to France to New York, Koko master, D' Banj anakuja na documentary ya dakika 90 inayohusu hustle zake za kimuziki. Interviews za radio na tv, performances mbalibali na maisha yake ya kimuziki kwa ujumla yamewekwa katika doc hii inayoitwa "The Tales of Oliver Twist - The Documentary". The Boss himself Kanye West pia ametokelezea katika doc hii!

Chungulia hapa Documentary hiyo:

















LIL WAYNE ATOKA HOSPITALI!

Hatimaye 'Mirror' hitmaker Lil Wayne ameruhusiwa kutoka hospitalini, California's Cedars-Sinai Medical Center's intensive care unit (ICU) alikokuwa amelazwa kwa siku 6 zilizopita. Lil Wayne a.k.a Dwayne Carter alipatwa maswahibu hayo baada ya kubugia madawa ya kulevya aina ya 'codeine' kupitiliza mpaka kupoteza fahamu kabisa.

Young Money president Mack Maine alithibitisha kutolewa kwa Wayne kupitia akaunti yake ya twitter, ''Thanks to Cedar Sinai for everything!!! @LilTunechi has been officially been released and is headed home....God is great (sic)''. ''God Bless.my son just release frm hospital.thanks 4 all tha luv.YMCMB.Richgang (sic)''



 




GHARAMA ZA WASANII HAWA KUPIGA SHOW NI NOMA!

Tajiri la kutupwa huko South Afrika,  Vivian Imerman amemchomolea msanii Adele toka Uingereza ku-perform katika harusi ya binti yake, Megan kutokana na gharama za msanii huyo kuwa juu mno. British singer Adele anahitaji pauni milioni 2.5 ili kutua South Africa na kupiga show hiyo. Hii ina maana kuwa kwa dakika 1 Adele anahitaji kulipwa pauni laki 1 na kwa vile show yake ilihitajika kuchukua dakika 25 hivyo ghararma yake ikawa pauni milioni 2.5!

Ikumbukwe miaka 2 iliyopita Taikuni hili lilimlipa Amy Winehouse maelfu ya dolari kwa ajili ya ku-perform katika harusi ya dada yake Megan, Bianca na alitarajia hivyo kwa Adele lakini alishangazwa kwa bei juu aliyoitaka Adele. Lakini dhamara ya  Vivian Imerman iko palepale na sasa anasaka msanii mwingine tofauti na Adele!


Adele
Wasanii wengine pamoja na gharama zao za kupiga show ni kama ifuatavyo:-
1. Jay Z & kanye West - $3,000,000
2. 50 Cent - $2,000,000
3. Eminem - $1,650,000
4. Rihanna - $800,000
5. Lil Wayne -  $500,000
6. Drake - $155,000
7. Nicki Minaj - $150,000
8. Akon - $120,000
9. T.I. - $110,000
10. Snoop Dogg - $105,000