Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 24 January 2013

EDEN HAZARD APAMSUA MBAVU MWOKOTA MIPIRA

Ni dakika ya 80 katika mchezo wa marudiano, nusu fainali ya kombe la ligi Capital One, kati ya Swansea na Chelsea. Winga wa Chelsea Eden Hazard,22, anafanya tukio la aibu hasa katika mpira wa miguu kwa kumbutua mwokota mipira na kumsababishia maumivu mbavuni na kuoneshwa kadi nyekundu. Dogo huyo aitwaye Charlie Morgan, 17, ni mtoto wa bosi wa Swansea, Martin Morgan. 

Hazard akiongea na Chelsea Tv baada ya mchezo alisema, "Dogo alilalia mpira na nilitaka kuuchukua mpira na haikuwa dhamira yangu kumdhuru, Niliupiga mpira na sio yeye. Naomba radhi. Dogo alikuja vyumba vya kubadilishia nguo na niliongea naye, aliniomba msamaha nami pia nilimtaka radhi" 

Swansea captain Ashley Williams, aliyekuwa karibu na tukio alisema, ‘Demba Ba alisema alimwona Hazard akimpiga dogo mbavuni. Huwezi fanya vile kwa dogo kama yule"

Chelsea manager Rafael Benitez, amesema kuwa suala hilo litashughulikiwa na klabu na tayari Hazard na dogo walikutana dressing room na kuombana msamaha. Police wa South Wales wanachunguza tukio hilo kwa umakini.


Japo Swansea walilazimishwa suluhu ya 0-0 lakini wamefuzu kwa faida ya magoli 2 ya mchezo wa awali na kuingia fainali Wembley baada ya miaka 100!


Eden Hazard katika purukushani na dogo
Demba Ba akimpoza dogo
Patashika: Captain wa Swansea Ashley Williams (katikati) aliyeshikiliwa akitaka kumzingua Eden Hazard
Red card: Eden Hazard nje
Dogo akiugulia
Dogo akipelekwa hospitali







PETER WA P-SQUARE APATA MTOTO WA PILI!

Hivi majuzi katika hospitali moja huko US of A, Peter Okoye, pacha katika kundi la P-Square alipata mtoto wa kike toka kwa girlfriend wake wa muda mrefu, Lola Omotoya. Peter aliandika katika ukurasa wake wa twitter na kutangaza mtoto wake huyo wa kike ataitwa Aliona.

Peter na Lola sasa wana watoto wawili, wa kwanza wa kiume aitwaye Cameron, 4, na wa pili wa kike Aliona! The family is now 'complete"!

Peter's girlfriend Lola Omotoya na bintiye Aliona

Peter Okoye


Peter na madaktari