Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday 6 April 2013

VIMINI MARUFUKU UGANDA!

Serikali ya Uganda iko mbioni kupeleka muswaada bungeni ili kupitisha sheria itakayo kataza wakina dada na kina mama kuvaa nguo fupi, kama vimini. Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo jirani, Bw. Simon Likodo ametoa tamko hilo akisema kuwa mwanamke yeyote atayevaa nguo itakayoonyesha maeneo yake nyeti atakuwa amevunja sheria na ataadhibiwa.
Waziri huyu ambaye ni Padre wa zamami wa Kanisani aligusia pia suala la picha chafu za ngono na kusema, "Serikali itaweka system itakayotambua raia yupi kaingia kwenye mtandao upi na hivyo kumtambua ni nani kaangalia picha chafu, 'pornographic pictures'.

Hii inamaanisha kuwa hata wasanii kama Beyonce na Madonna watapigwa marufuku kuja Uganda. Pia luninga za Uganda hazitaruhusiwa kuonyesha picha chafu zenye kuonysha maungo ya mwanamke.

Adhabu kwa mwanamke atapatikana na hatia ya kuvaa nguo fupi atapigwa faini ya Shilingi za Kiganda milioni 10 sawa na pauni 2,500. Au miaka 10 jela! Waganda wengi wako kinyume na kupitia mitandao ya facebook na twitter wameendesha kampeni '#SaveMiniSkrt' inayolenga kupinga muswaada huu!