Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday 12 April 2013

AKON AMPONGEZA KENYATTA, AKOSOLEWA!

Baada ya kuapishwa na kuwa raisi kamili, pongezi mbalimbali zimekuwa zikitolewa na mmoja wa watu maarufu ambao hawakuwa nyuma kusifia jinsi mchakato mzima wa uchaguzi ulivyokwenda kwa amani na utulivu mpaka kupatikana kwa raisi Uhuru Kenyatta ni Akon. Baada ya hapo sasa zikatoka comments mbalimbali katika fanpage yake ambazo Akon alizipotezea lakini hii hakuiacha iende hivihivi.


Mmoja wa commenters aliandika hivi, "Huyu (Kenyatta) ni mwizi kama baba yake. Aliiba ardhi na kabila lake tu ndilo lililompigia kura. Kwa sasa ana kesi katika mahakama ya kimataifa na naamini watamtia hatiani. Kwanini (Akon) umpongeze?????"

Ndipo Akon akajibu, "Ndio maana Africa haiwezi kusonga mbele. Tunapoteza muda mwingi katika vitu visivyo na maana. Nimempongeza kwa kufanya uchaguzi kwa njia ya amani! Hii ni hatua kubwa kwa Afrika. Kama kuna lolote baya alilolifanya hapo nyuma ni yeye (Kenyatta) ataenda kujibu kwa Mungu. Sasa kwa kwanini ujiumize kichwa? Sisi sio watu wa kumjaji!"




REEBOK WAMTEMA RICK ROSS BAADA YA KUBAKA!

Hatimaye kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo Reebok imemtema rasmi Rick Ross. Hii ni baada ya the Maybach Music rapper The Boss kutema lines zenye utata tena zenye kumzalilisha mwanamke na kuonekana kama alibaka mwanamke kwa mistari yake katika ngoma ya "U.O.E.N.O".

Mistari ya Rossay inasomeka, ‘Put molly all in her champagne, she ain’t even know it/I took her home and I enjoyed that, she ain’t even know it’. Akimaanisha anamuwekea molly (kilevi) kwenye kinywaji/shampeni ya demu bila yeye kujua. Anampeleka nyumbani kwake na kum-do bila yeye (demu) kujua.
Wanaharakati waliowahi kubakwa juzi kati waliandamana mpaka ofisi za Reebok kuwaomba waache kumdhamini Rossay na Reebok leo hii wametoa tamko kuachana rasmi na rapper huyo na kusikitishwa kwa kile Rossay alichokifanya katikam ngoma hiyo ya Rocko.