Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday 21 May 2013

WASANII HAWA WATAPAFOMU UFUNGUZI WA BIG BROTHER AFRICA JUMAPILI HII!

Moja kati ya Tv reality shows kubwa Africa itaanza kuruka hewani Jumapili hii. Hii ni Big brother Africa 'The Chase'. Kama ulivyo utmaduni wa BBA ni lazima shamra shamra za ufunguzi wa shindano hili uambatane na show kali toka kwa sanii wakali hapa africa au nje. na wasanii watafungua shindano hili kwa mwaka 2013 tayari wameshatajwa.



Kutoka Afrika Mashariki, Kisima award winning star STL amebahatika ku-grace the stage pamoja na wasanii toka Afrika Kusini kama Mafikizolo. Toka Naija Don Jazzy B atafanya yake siku hiyo bila kumsahau Wande coal! Show itaanza saa 1:00 kwa midaya afrika ya Kati na kurushwa live na channels za DSTV!
STL

D' BANJ APIGA SHOW NA VIATU TOFAUTI!

The koko master himself D’banj ametokelezea na kituko cha kipeke yake on stage. This time arround, D' Banj alipanda na ku-perfom katika stage ya MTV All Stars concert huko Durban, South Africa akiwa na raba (sneakers) mbili tofauti miguuni mwake. Moja ikiwa ni nyeupe na nyingine ni nyeusi lakini zote ni aina ya Guiseppe Zanotti.

Hata hapa Bongo kamchezo haka kalishawahi fanywa na rapa controversial Ney wa Mitego kwa kutupia viatu tofauti katika videos kadhaa na katika shows mbalimbali pia.
D’banj
 

PROFFESOR JAY AJIUNGA NA CHADEMA.

Mambo sasa yamebadilika. Msanii nguli wa Hip-hop na bongo flava  Joseph Haule a.k.a Proffesor Jay, leo hii amejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na tayari amekabidhiwa kadi yake ya uanachama. Swali linalobaki vichwani mwa watu na mashabiki wa muziki Tanzania ni kuwa Je, Prof. Jay atagombea ubunge kupitia chama hicho kama ilivyokuwa kwa swahiba wake walioanza nae muziki kitambo hicho, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu?

Prof. Jay anaongeza idadi ya wanamuziki walioamua kuingia rasmi katika siasa akitanguliwa na wasanii kama Kalapina (CUF), Mwana-FA (CCM), Sugu (Mb. Mbeya-CHADEMA)


Prof. Jay na Sugu