Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday 23 May 2013

ZITTO AMPOTEZEA DIVA!

Pamoja na Diva Loveness Love kutangaza kumpiga chini Mheshimiwa mbunge Zitto Kabwe na kuendelea kumsakama kwa maswali kadhaa na jumbe mbalimbali kupitia akaunti yake ya Instagram na mitandao mingine, lakini mheshiwa ameonyesha ustaarabu kwa kuamua kujikalia kimya bila kumjibu lolote bi-dada huyo.



Haya yote yamejitokeza hasa wakati huu ambapo The Romantic voice Clouds Fm presenter wa 'Ala za Roho' Diva amemdondokea msanii mwenye mkwanja mrefu toka area code 254, 'Kerewa' hitmaker Prezzo na kwa mujibu wa Diva ni kuwa penzi lao liko moto bati!

Tuesday 21 May 2013

WASANII HAWA WATAPAFOMU UFUNGUZI WA BIG BROTHER AFRICA JUMAPILI HII!

Moja kati ya Tv reality shows kubwa Africa itaanza kuruka hewani Jumapili hii. Hii ni Big brother Africa 'The Chase'. Kama ulivyo utmaduni wa BBA ni lazima shamra shamra za ufunguzi wa shindano hili uambatane na show kali toka kwa sanii wakali hapa africa au nje. na wasanii watafungua shindano hili kwa mwaka 2013 tayari wameshatajwa.



Kutoka Afrika Mashariki, Kisima award winning star STL amebahatika ku-grace the stage pamoja na wasanii toka Afrika Kusini kama Mafikizolo. Toka Naija Don Jazzy B atafanya yake siku hiyo bila kumsahau Wande coal! Show itaanza saa 1:00 kwa midaya afrika ya Kati na kurushwa live na channels za DSTV!
STL

D' BANJ APIGA SHOW NA VIATU TOFAUTI!

The koko master himself D’banj ametokelezea na kituko cha kipeke yake on stage. This time arround, D' Banj alipanda na ku-perfom katika stage ya MTV All Stars concert huko Durban, South Africa akiwa na raba (sneakers) mbili tofauti miguuni mwake. Moja ikiwa ni nyeupe na nyingine ni nyeusi lakini zote ni aina ya Guiseppe Zanotti.

Hata hapa Bongo kamchezo haka kalishawahi fanywa na rapa controversial Ney wa Mitego kwa kutupia viatu tofauti katika videos kadhaa na katika shows mbalimbali pia.
D’banj
 

PROFFESOR JAY AJIUNGA NA CHADEMA.

Mambo sasa yamebadilika. Msanii nguli wa Hip-hop na bongo flava  Joseph Haule a.k.a Proffesor Jay, leo hii amejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na tayari amekabidhiwa kadi yake ya uanachama. Swali linalobaki vichwani mwa watu na mashabiki wa muziki Tanzania ni kuwa Je, Prof. Jay atagombea ubunge kupitia chama hicho kama ilivyokuwa kwa swahiba wake walioanza nae muziki kitambo hicho, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu?

Prof. Jay anaongeza idadi ya wanamuziki walioamua kuingia rasmi katika siasa akitanguliwa na wasanii kama Kalapina (CUF), Mwana-FA (CCM), Sugu (Mb. Mbeya-CHADEMA)


Prof. Jay na Sugu

 
 
 

Monday 20 May 2013

JCB AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA MZUNGU!

Mwanahip-hop toka A-Town, 'Ukiskia paah' hitmaker single, JCB ameachana na ukapera this week-end kwa kufunga ndoa. Na hizi ni baadhi ya picha za harusi hiyo iliyofanyika Arusha Jumamosi hii!



 

SIKILIZA HOTUBA YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE KUHAIRISHWA LEO HII!


Friday 17 May 2013

MNYAMA AMPOTEZEA ANACONDA

TID a.k.a Mnyama amemtema au amemtolea nje Lady Jay Dee a.k.a anaconda kushiriki katika show yake ya kutimiza miaka 13 katika mziki pale Nyumbani Lounge mwishoni mwa mwezi huu. Hii inakuja baada ya Jay Dee kuingia katika mzozo mkubwa na Mkurugenzi utafiti wa redio binafsi, Clouds Fm, Ruge Mutahaba!
 
Katika kuthibitisha kwake kutoshiriki show hiyo, TID aliandika hivi katika ukurasa wake wa facebook:-
“Three reasons why I can’t do Lady Jay Dee Show….. No 1 I have better contract which pays me better than. No 2 I really don’t want to be between anybody’s conflict, ya kwangu yananishinda naona niepushe shari. No3 nataka kuoa muda wangu ndio huu………. Kama nimekukosea captein na madame kazeni but I have been tru the same shit”
 
TID anaungana na wasanii kama Linah, Barnaba na Matonya ambao walishatangaza hapo wali kuwa hawatashiriki kabisa katika show hiyo. Amebaki Professor Jay.
 
 

Thursday 16 May 2013

D' BANJ ALA SAHANI MOJA NA BARNABA BOY

Wakati wasanii wa Kibongo wakihaha kutafuta michongo mbalimbali ya kuwaingiza mkwanja ikiwemo kupata haki sahihi ya umiliki wa ringtones zao na zaidi kupata mashavu ya kuwa mabalozi wa makampuni mbalimbali, huko kwa wenzetu hasa West Africa wameshapiga hatua kubwa sana katika hili.

Achilia mbali tuzo lukuki na hits anazozidondosha siku baada ya siku, neema zinaonekana bado kumdondokea artiste huyu kwani leo hii KokoMaster a.k.a D’ Banj alisaini mkataba wa kuwa balozi wa benki moja huko Naija iitwayo Bank of Industry.
Ms Evelyn Oputu, Managing Director & Chief Executive Officer of Bank of Industry na balozi D' Banj


 
Hapa Tanzania hii imekuwa hatua mpya sasa hasa kwa upande wa mabenki kuwachagua wasanii wazawa kuwa mabalozi wake na mfano hai tu ambao kidogo unaendaana na huo wa msanii kuwa balozi ni wa Barbana Boy kufanya kazi na benki ya Barclays Tanzania (japo Barnabas si balozi wa benki hiyo) lakini cha msingi ni lile dili tu kati yake na benki hiyo ambapo Barnabas ataingiza zaidi ya dola za Kimarekani 20,000/=kwa kuimba wimbo juu ya wanawake wa Kitanzania.



Tuesday 14 May 2013

MZUNGU AWAFANYISHA NGONO WANAWAKE 11 NA MBWA WAKE

Kutoka Mombasa, Kenya mzungu mmoja aliyetambulika kwa jina la Christopher Clement Weisssenrieder  raia wa Switzeland  ametiwa mbaroni baada ya kuwafanyisha ngono wanawake 11 na mbwa wake na kuwarekodi.

Haya ndio majina yao ya wanawake hao:
  1. Janet Akoth Omollo,
  2. Mercy Waithera Karanja,
  3. Mary Nyambura Kimani,
  4. Magdaline Wairimu Chege,
  5. Celestine Nekesa Sitati
  6. Dorcus Melishah Indakwa
  7. Lydia Nyaboke Momanyi,
  8. Philidelia Mawia Solomon,
  9. Anne Wanjiku Gichuki


BEYONCE ANA UJAUZITO TENA!

Mtandao wa NY Post umeibuka na ripoti kuwa mke wa Jay Z, Beyonce anatarajia mtoto wa pili kwa kuwa sasa hivi ana ujauzito! Beyonce ambaye sasa hivi yupo katika tour ndefu ya kimuziki juzi akti alionekana kitumbo kimetokeza alipotupia kigauni akizungushia na mkanda kiunoni. Blogs mbalimbali pia zimetoa picha kadhaa zinazoonyesha vizuri eneo la tumbo la Bey kuwa sasa mabo yamejipa tayari kumpokea mtoto wa pili!


JAY Z KUPIGA SHOW DAR OCTOBA 4

Jay Z ametoa mlolongo wa shows zake atakazopiga kwa wiki 7 kuizunguka dunia kwa dhumuni la kuleta ufahamu juu ya tatizo la maji. Tour hii ndefu itaanza Septemba 9 huko Krakow, Poland. Jay Z atadondoka Dar na atagonga show hiyo tarehe 4 Octoba pale Diamond Jubilee. Na hii ndio list ndefu ya tour ya Jay Z:-


Sept. 9: Krakow, Poland (Coca-Cola SW Live Festival)
Sept. 10: Bratislava, Slovakia (Incheba)
Sept. 15: Amsterdam (Heineken Music Hall)
Sept. 16: Germany (TBA)
Sept. 18: Istanbul (Refresh the Venue)
Sept. 19: Athens (Olympic Arena)
Sept. 21: Manchester, England (Evening News Arena)
Sept. 22: Glasgow (SECC)
Sept. 23: Birmingham, England (National Indoor Arena)
Sept. 24: London (Wembley Arena)
Sept. 26: Dublin (the Point)
Sept. 27: London (Royal Albert Hall)
Sept. 29: Paris (Le Zenith)
Sept. 30: Milan (Fiera di Milano)
Oct. 2: Barcelona (Teatro Heineken)
Oct. 4: Dar es Salaam, Tanzania (Diamond Jubilee)
Oct. 6: Accra, Ghana (Accra Conference Center)
Oct. 7: Lagos, Nigeria (Ocean View)
Oct. 9: Luanda, Angola (Cine Karl Max)
Oct. 11: Cape Town, South Africa (Belleville Velodrome)
Oct. 13: Durban, South Africa (ABSA Stadium Outer Fields)
Oct. 14: Johannesburg (Coca Cola Dome)
Oct. 17: Hong Kong (TBA)
Oct. 18: Bangkok, Thailand (BEC Tero Hall)
Oct. 20: Seoul, Korea (Walker Hill Gayagum Concert Hall)
Oct. 21: Taipei, Taiwan (Taipei Dome)
Oct. 23: Singapore, Singapore (Suntec City Concert Hall)
Oct. 25: Sydney (Entertainment Centre)
Oct. 27: Brisbane, Australia (Entertainment Centre)
Oct. 28: Melbourne (Rod Laver Arena)



Thursday 9 May 2013

LADY JAY DEE KUJIBU MAPIGO YA RUGE KESHO.

Kufuatia majibu ya Ruge Mutahaba kwa Lady Jay Dee hivi majuzi kupitia redio yake binafsi ya Clouds Fm 'Super Brand', kesho asubuhi katika kipindi cha Sunrise cha Times Fm 100.5 Lady Jay Dee a.k.a Anaconda atarudisha mapigo kwa kujibu maswali yote au hoja zote zilizowekwa mezani na Ruge. Zaidi ya hapo Jay Dee ameahidi kuibua mapya kabisa ambayo hajawahi kuyasema hapo kabla.


Wednesday 8 May 2013

NICKI MINAJ APIGA PICHA UCHI KATIKA GAZETI!

US rapper and entertainer, Nicki Minaj alisaula nguo zote katika upigaji picha wa gazeti la KING huko USA. Haijafahamika ni kiasi gani cha mkwanja Minaj amevuta lakini it is to be a huge bundle of money!



JA RULE ATOKA JELA

Rapper Jeffrey Atkins a.k.a Ja Rule ameachiwa huru toka jela ya Ray Brook Federal Prison huko New York siku ya Jumanne asubuhi (07 May 2013). Lakini Ja Rule amepewa sharti la kukaa nyumbani (kifungo cha nyumbani) mpaka tarehe 28 July.

Ja Rule alihukumiwa kwenda jela miaka 2 mnamo mwaka 2010 baada ya kukutwa na hatia ya kumiliki silaha bila kibali. Mwezi mmoja baada ya kuanza kutumikia kifungo chake, mnamo June, 2011 alikutwa na hatia nyingine ya kukwepa kulipa kodi na hapo ndipo akaongezewa miezi 28 jela!
 




Monday 6 May 2013

PAUL WA P-SQUARE AKATAA MTOTO WA PILI!

Katika kipindi kisichopungua mwezi mmoja, Paul Okoye amepata mtoto wa pili, tarehe 11 April demu wake wa siku nyingi, Anita alijifungua mtoto wa kiume, Andre Paul Okoye. Na sasa kuna taarifa zinasema kuwa demu wake mwingine, Elshama Benson Igbanoi, 19, amejifungua mtoto wa kiume huko Queen Charlotte and Chelsea Hospital, London na kupewa jina la Michelle Paul Okoye.
Michelle Paul Okoye
Chakushangaza Paul amemkataa mtoto huyo huku akiahidi kutua London ili kufanya DNA test kabla ya kukubali wajibu wake kwa mtoto kama baba. Baba wa binti huyo, Mzee Igbanoi amesema kuwa ameshamtumia e-mails za kutosha Paul toka binti yake akiwa mjamzito mpaka anajifungua lakini Paul hajajibu lolote.

Kuona hivyo Familia ya Mzee Igbanoi imeshafanya utaratibu wa kuwasiliana na Baba na Shangazi wa Paul huku akikazia kuwa binti yake hajawahi kuwa na mwanaume mwingine isipokuwa msanii huyo Paul Okoye ambaye ndiye alimtoa bikira Elshama akiwa na umri wa miaka 17.

Elshama
Mpaka sasa bado gharama za hospitali zinazozidi pauni 5,000 hazijalipwa na Elshama. Inasemekana kuwa Elshama ni rafiki pia wa Anita, msichana aliyemzalia huyuhuyu Paul Okoye mtoto wa kwanza tarehe 11 mwezi huu!

Paul Okoye na mtoto wake wa kwanza, Andre Okoye

Saturday 4 May 2013

JUSTIN BIEBER ASIMAMISHA SHOW KUPISHA SWALA

Kipenzi cha walimbwende, Justin Bieber juzi Alhamiis alisimamisha show yake ili kupisha waumini wa dini ya Kiislamu kuswali (Waumini wa dini hiyo huswali mara tano kwa siku). Na baada ya swala dogo aliendeleza makamuzi kama kawaida. Hii ilitokea jijini Istanbul, Uturuki katika concert iliyofanyika Technical University sports arena.
Kupitia akaunti mbalimbali twitter za mashabiki wake walipendezeshwa na tukio hilo na kuandika hivi:-
Photo - Justin Bieber Stops Concert For Muslim Prayer
Pamoja na hayo bado Justin Bieber amekutana na vikwazo mbalimbali katika nchini za Kiarabu vikiwemo kufutwa kwa show yake huko Oman  kwa vile shows zake huchochea ngono kwa vijana!
 
 

JENGO LINALOFANANA NA UUME NCHINI CHINA.

Jengo hilo lenye urefu wa mita 150, hivi sasa bado linaendelea kujengwa jijini Beijing. Kutokana na muundo huo usiokua wa kawaida, picha za kibunifu zikaanza kuibuka katika website ambayo ni kama “Twitter ya China,” inayoitwa Sina Weibo.

Watu wengi wameeleza kuwa kwa kutumia ubunifu kidogo tu wa photoshopping, unaweza kuambatanisha picha ya jengo hilo, ambalo raia wamelipa nickname “Giant Penis” au “Uume mkubwa,” katikati ya “miguu” ya jengo lingine maarufu nchini humo ambalo ni makao makuu ya kituo cha TV cha China Central Television (CCTV,) almaarufu kama  “Big Underpants” building au Jengo la Chupi Kubwa.


Habari za utani huo zilifikia wakubwa nchini humo ambao walikerwa na kuamua kuwaharibia watu raha zao kwa kuamuru website ya Sino Weibo ku-block search zote zinazotafuta picha au habari za jengo hilo. Kwa sasa Wachina wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe “kuendana na sheria, kanuni na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search results) hayawezi kuonyeshwa.


Mwandishi wa Reuters Anita Li amesema “hii inaonyesha frustrations miongoni mwa vijana watumiaji wa internet nchini China, na pia inaonyesha ni kiasi gani “wakubwa” wako sensitive kwa hata vitu vidogo vya kipuuzi online.”


Friday 3 May 2013

RUGE MUTAHABA KUJIBU MAPIGO YA LADY JAY DEE!

Hatimaye mtuhumiwa namba moja kulingana na shutuma au tuhuma kadhaa alizokuwa akituhumiwa kwa takribani mwezi mmoja sasa na Lady Jay Dee, Mkurugenzi wa Clouds FM Ruge Mutahaba kwa mara ya kwanza atafungua mdomo wake siku ya Jumatatu asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast ili kujibu tuhuma hizo!

Tayari mpaka sasa Jay Dee a.k.a Anakonda alishasema mambo kadha wa kadha akielekeza tuhuma kwa mmiliki Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba. Baadhi ya tuhuma za Lady Jay Dee kupitia akaunti yake ya twitter na blogspot yake ni kutopigwa nyimbo zake redioni Clouds Fm, kuingiliwa katika shows zake na hata kuwakataza baadhi ya wasanii hasa wale wa THT kutoshirikiana na Lady Jay Dee. 

Bifu lao hili limefika pabaya mpaka kufikia Jay Dee kutangaza kuwa hata akifa si Kusaga wala Ruge wasifike mazikoni na kuacha usia kuwa atakayewaona basi awatupie mawe!










BAADA YA KUUJAZA UWANJA, SASA WAPEWA JINA LA DR. CHAMELEON!

Hii haijawahi kutokea huko Uganda kwa local artistes. Show ya uzinduzi wa album ya ‘Badilisha’ ya Mfalme Doctor Chameleon iliyofanyika wiki iliyopita ndiyo mpaka sasa inayokamata namba moja kwa kuujaza uwanja huu wa Rugby, Kyaddondo Rugby grounds! Wamiliki wa huu uwanja wakaona isiwe tatizo, wakaamua kufuta jina la uwanja na sasa uwanja huu unaitwa Jose Chameleon Rugby grounds!

Siku ya show ya ‘Badilisha’, toka saa 10 jioni kulikuwa na foleni ya hatari ya raia na mpaka kufika saa 1 usiku, uwanja ulikuwa ushatema na watu elfu kumi walikuwa tayari wapo uwanjani kwa uzinduzi huo!

Bebe Cool the Prince ndio anafuata kwa kuujaza uwanja huo alipozindua albam yake ya ‘Kamwako’ na watatu ni The Novice Bobi kupitia albam yake ya ‘Tugambire Ku Jennifer’ ambapo aliingiza watu elfu 8.