Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday 3 May 2013

RUGE MUTAHABA KUJIBU MAPIGO YA LADY JAY DEE!

Hatimaye mtuhumiwa namba moja kulingana na shutuma au tuhuma kadhaa alizokuwa akituhumiwa kwa takribani mwezi mmoja sasa na Lady Jay Dee, Mkurugenzi wa Clouds FM Ruge Mutahaba kwa mara ya kwanza atafungua mdomo wake siku ya Jumatatu asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast ili kujibu tuhuma hizo!

Tayari mpaka sasa Jay Dee a.k.a Anakonda alishasema mambo kadha wa kadha akielekeza tuhuma kwa mmiliki Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba. Baadhi ya tuhuma za Lady Jay Dee kupitia akaunti yake ya twitter na blogspot yake ni kutopigwa nyimbo zake redioni Clouds Fm, kuingiliwa katika shows zake na hata kuwakataza baadhi ya wasanii hasa wale wa THT kutoshirikiana na Lady Jay Dee. 

Bifu lao hili limefika pabaya mpaka kufikia Jay Dee kutangaza kuwa hata akifa si Kusaga wala Ruge wasifike mazikoni na kuacha usia kuwa atakayewaona basi awatupie mawe!










No comments:

Post a Comment