Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday 3 May 2013

BAADA YA KUUJAZA UWANJA, SASA WAPEWA JINA LA DR. CHAMELEON!

Hii haijawahi kutokea huko Uganda kwa local artistes. Show ya uzinduzi wa album ya ‘Badilisha’ ya Mfalme Doctor Chameleon iliyofanyika wiki iliyopita ndiyo mpaka sasa inayokamata namba moja kwa kuujaza uwanja huu wa Rugby, Kyaddondo Rugby grounds! Wamiliki wa huu uwanja wakaona isiwe tatizo, wakaamua kufuta jina la uwanja na sasa uwanja huu unaitwa Jose Chameleon Rugby grounds!

Siku ya show ya ‘Badilisha’, toka saa 10 jioni kulikuwa na foleni ya hatari ya raia na mpaka kufika saa 1 usiku, uwanja ulikuwa ushatema na watu elfu kumi walikuwa tayari wapo uwanjani kwa uzinduzi huo!

Bebe Cool the Prince ndio anafuata kwa kuujaza uwanja huo alipozindua albam yake ya ‘Kamwako’ na watatu ni The Novice Bobi kupitia albam yake ya ‘Tugambire Ku Jennifer’ ambapo aliingiza watu elfu 8.


No comments:

Post a Comment