Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday 24 July 2013

NYAKATI MBILI MBAYA ZA BEYONCE!

Hii ilikuwa ni tour yake iitwayo 'B-Day tour' akiperform 'Ring the Alarm'. Hapa alidondoka mzima mzima wakati akipanda ngazi za steji.


Katikati ya show yake ya mwezi March mwaka huu, Beyonce alimpa microphone shabiki wake aliyekuwa na midadi kwelikweli, ili nae aimbe kidogo japo mistari miwili mitatu. Kumbe jamaa hajui lolote. Shabiki huyo,  Princess Eugenie alipopewa mic aligeuka bubu ghafla. Whoops!


WASANII WATANO WASIOJUA KUIMBA JAPO MASHABIKI WANAWAKUBALI!

1.KEYSHIA COLE
Inatakiwa atafutwe mtu amwambie binti huyu wa Frankie kuwa sauti yake haijakaa sawa. Ni lazima atafute mwalimu wa sauti ili amuweke sawa.


2.ALICIA KEYS
Baada ya kuzaa, Alicia amerudi tena kuwa mzuri ajabu kimuonekano. Lakini kiumbaji hasa vocally, wataalam wa mziki wanasema ameshuka sana. Na hii ni baada ya kuambatana na mumewe Swizz Beatz. Sauti yake haijarudi na kuwa tamu tena.

3.JUSTIN BIEBER
Ana uwezo mzuri wa kulimiliki jukwaa lakini linapokuja suala la sauti, Bieber hamgusi Usher hata Maxwell. Kwa mwendo huu miaka kumi toka sasa anaweza kuwa amesahaulika.


4. MICHELLE WILLIAMS
Michelle anaboa sana. Sauti yake bado haijawa ile ya kuweza kumuweka katika list ya waimbaji bora USA kutokana na vile ana pata shida sana kufikia nota za juu katika uimbaji wake. Alikuwa memba wa Destiny child. Pengine hii ndio sababu iliyomfanya asionekana kung'aa katika kundi hilo lililovunjika na hata kupotea kabisa tofauti na Beyonce na Kelly Rowland. 


5. ROBIN THICKE
Robin anaonekana mlazimishaji kwelikweli. Anataka kwenda high notes lakini hafiki inavyotakiwa kimuziki. Tafura performace yake ya BET 2013.