Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Friday 17 August 2012

PAH ONE NA CAMP MULLA WANAUFANANO

Japo si haki kuyalinganisha makundi haya kwa kuzingatia mafanikio na umaarufu kutokana na ukweli kwamba Camp Mulla wapo mbali zaidi na wanajulikana kimataifa kuliko Pah One, kuna mengi yakufanana katika makundi haya mawili. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa yote ni coincidence tu na hakuna lililoiga kundi jingine. Pah One wanawakilisha Tanzania na Camp Mulla wanawakilisha Kenya. 


Haya ni mambo kumi wanayofanana:

1. Makundi yote  yaliundwa miaka miwili ama mitatu iliyopita

2.Makundi yao yanaundwa na waimbaji/marapper wanne

PahOne – Aika, Ola, Nah Reel na Igwe

Camp Mulla - Taio Tripper, Shappa Man, Miss Karun, K'Cous , Japo yupo pia
Mykie Tuch ambaye ni CEO

Camp Mulla
3.Kila kundi lina wavulana watatu na msichana mmoja

PahOne – Aika

CampMulla -  Miss Karun

4. Kila kundi lina producer ambaye ni member pia na nyimbo zao hutengeneza wenyewe

PahOne – Nah Reel
Camp Mulla - K'Cous na Shappa Man


5. Wengi wana miaka chini ya 25

6. Wengi bado wanasoma

7. Karibu wote wanatokea kwenye familia bora
Pah One – Ola na Igwe wamesomea Afrika Kusini , Aika na Nah Reel wamesomea India

Camp Mulla – Mtandao mmoja uliwahi kuwaponda kuwa wanapendelewa kwakuwa wanatoka kwenye familia bora

Pah One
8. Muziki wanaofanya ni wa aina moja (Hip hop, dance na aina zingine za muziki wa kisasa)

9. Uvaaji wao unafanana sana

10. Wote wana akaunti maarufu ya mtandao wa muziki wa Reverbnation

No comments:

Post a Comment