Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday 27 August 2012

BBC DIRA YA DUNIA KURUKA LIVE LEO KWENYE TV

Saleem Kikeke

Matangazo ya televisheni ya Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC leo yanaanza kuruka rasmi kupitia Star TV ya Tanzania na Qtv ya Kenya.

Wiki iliyopita kulifanyika uzinduzi wa matangazo hayo jijini Dar es Salaam.

Matangazo hayo ya Dira ya Dunia kwa upande wa radio ni maarufu zaidi pengine kuliko matangazo yote ya radio za kimataifa zinazotangaza Kiswahili duniani.

Kuingia kwenye matangazo ya runinga kwa BBC Swahili kunafungua ukurasa mpya wa matangazo ya aina hiyo ya Kiswahili nchini.

BBC Dira ya Dunia siku za usoni itakuwa ikishindana na matangazo mengine ya Kiswahili ya Al-Jazeera ambayo yapo kwenye mchakato wa kuanzishwa.


No comments:

Post a Comment