Hatimaye kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo Reebok
imemtema rasmi Rick Ross. Hii ni baada ya the Maybach Music rapper The Boss kutema lines zenye utata tena
zenye kumzalilisha mwanamke na kuonekana kama alibaka mwanamke kwa mistari yake
katika ngoma ya "U.O.E.N.O".
Mistari ya Rossay inasomeka, ‘Put molly all in her champagne, she ain’t even know it/I
took her home and I enjoyed that, she ain’t even know it’. Akimaanisha anamuwekea molly (kilevi) kwenye kinywaji/shampeni ya demu bila
yeye kujua. Anampeleka nyumbani kwake na kum-do bila yeye (demu) kujua.
Wanaharakati waliowahi kubakwa juzi kati waliandamana mpaka ofisi za Reebok kuwaomba waache kumdhamini Rossay na Reebok leo hii wametoa tamko kuachana rasmi na rapper huyo na kusikitishwa kwa kile Rossay alichokifanya katikam ngoma hiyo ya Rocko.