Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday, 9 April 2013

AVRIL KUUZA MADAWA YA KULEVYA!

Singer now turning to be an actress Avril amekula mchongo wa ku-act katika tamthiliya ya 'Noose of Gold’ inayorushwa na kituo cha M-NET. Avril ataigiza katika season ya 5 ya tamthiliya hiyo na nafasi yake ni ‘Muuza madawa ya kulevya’.

Avril alipoulizwa kama nafasi hiyo inaakisi maisha yake ya kawaida ya kila siku, alikana kwa kusema, “Sijawahi kuhusika iwe kwa kutumia au kuuza madawa ya kulevya. Sasa hivi ndio najifunza mambo haya”.

Pengine nafasi hii imekuja baada ya kuonekana amefanya vizuri sana kiuigizaji katika video ya 'Kesho' ya Diamond.
 

 
 


RAISI WA URUSI AONYESHWA MATITI ZIARANI HADHARAN!


Raisi wa Urusi Vladimir Putin na Chancellor wa Ujerumani, Bi. Angela Merkel walikutana na kimbwanga cha mwaka baada ya kuvamiwa na mwanamke mwanaharakati aliyeku wazi kabisa kifuani na kuwaonyesha matiti yake viongozi hao walipokuwa katika ziara ya viwanda huko Hanover, Ujerumani jana Jumatatu.



Hata hivyo Bi. Angela Merkel hakufurahishwa na ulinzi mbovu hivyo kumruhusu mwanamke huyo kujipenyeza mpaka kuwafikia viongozi hao!


Cheki reaction ya bwana raisi baada ya kuonyeshwa matiti.

KANYE WEST AIBA NGOMA!


Roc-A-Fella Records & Good Music Rapper Kanye West, 35, ameingia matatani kwa kuiba baadhi ya mistari na kuitumia katika ngoma yake ‘Gold Digger’. Jana Jumatatu Trena Steward na Lorenzo Pryor, watoto wa David Pryor, ndio waliofungua kesi hii kwa niaba ya baba yao aliyeimba wimbo huo 'Bumpin Bus Stop' kwa kushirikiana na bendi yake, Thunder & Lightening mwaka 1974.
 
Ni sekunde 13 tu za wimbo wa David Pryor  ndio West alikopi mistari pia tune ambayo ni 'Get down' three times’ huku West alisema, 'Get down, girl, go head get down' three times’. Trena Steward na Lorenzo Pryor, watoto wa David Pryor kila mmoja anamiliki robo ya tune katika wimbo huu na wanahitaji fidia ya $ 150,000 pamoja gharama za wakili.

Hii sio mara ya kwanza kwa West kupelekwa mahakamani kwani  mwaka September, 2012, New York record label, TufAmerica ilimfungulia mashtaka West kwa kuchukua mistari ya ngoma ya Eddie Bo,  'My Beautiful Dark Twisted Fantasy' na kutoa ‘Stronger’.







Monday, 8 April 2013

A GAME TWO CAN PLAY! BROWN Vs RIHANNA.

Juzi Chris Brown alionekana anamhofia babyboo wake Rihanna kwamba anaweza kumsaliti wakati akiwa katika tour yake. Lakini inaonekana kama Rihanna ndio wakumhofia  Chris Brown wakati alipoonekana aki-party club na dada duu mmoja usiku wa Jumamosi! Brown alionekana akishikana mikono na mtoto huyo huku akimpa chupa moja ya champagne huko Los Angeles nightclub.


 
Wakati hayo yakitokea kwa Brown, Rihanna ,25, alionekana Jumapili (siku inayofuata) akicheki basketball match kati ya Los Angeles Clippers dhidi ya Los Angeles Lakers na mchizi mwingine kabisa!
 

 
Nani hapa anamdanganya mwenzake? Is it Brown or Riri?

Saturday, 6 April 2013

VIMINI MARUFUKU UGANDA!

Serikali ya Uganda iko mbioni kupeleka muswaada bungeni ili kupitisha sheria itakayo kataza wakina dada na kina mama kuvaa nguo fupi, kama vimini. Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo jirani, Bw. Simon Likodo ametoa tamko hilo akisema kuwa mwanamke yeyote atayevaa nguo itakayoonyesha maeneo yake nyeti atakuwa amevunja sheria na ataadhibiwa.
Waziri huyu ambaye ni Padre wa zamami wa Kanisani aligusia pia suala la picha chafu za ngono na kusema, "Serikali itaweka system itakayotambua raia yupi kaingia kwenye mtandao upi na hivyo kumtambua ni nani kaangalia picha chafu, 'pornographic pictures'.

Hii inamaanisha kuwa hata wasanii kama Beyonce na Madonna watapigwa marufuku kuja Uganda. Pia luninga za Uganda hazitaruhusiwa kuonyesha picha chafu zenye kuonysha maungo ya mwanamke.

Adhabu kwa mwanamke atapatikana na hatia ya kuvaa nguo fupi atapigwa faini ya Shilingi za Kiganda milioni 10 sawa na pauni 2,500. Au miaka 10 jela! Waganda wengi wako kinyume na kupitia mitandao ya facebook na twitter wameendesha kampeni '#SaveMiniSkrt' inayolenga kupinga muswaada huu!