Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Sunday, 17 February 2013

RIHANNA AJA NA MAVAZI YAKE!

Baada ya kujijengea jina kubwa katika ulimwengu wa muziki duniani sasa Rihanna anaenda extra mile kwa kuingia rasmi katika tasnia ya ubunifu wa mavazi! Kwa mara ya kwanza this Barbadian singer aliingiza style mpya ya mavazi katika wiki ya mavazi huko London, London Fashion Week, jana Jumamosi!



The Stay singer alipata mapokezi mazuri toka kwa mashabiki na hata watu mashuhuri akiwemo Toni Jones aliye-comment kuwa mavazi hayo ‘yanavutia’ na ‘kuvalika’ pia!

Mavazi ya Rihanna yamelenga zaidi kuvaliwa na vijana na hasa ameanza na wa kike!











Angalia kipande kidogo cha video ya show hiyo:

Saturday, 16 February 2013

KIM KARDASHIAN ATUA NIGERIA, AUZA MJENGO WAKE!


The reality Tv star Kim Kardashian ametua nchini Nigeria saa moja lililopita. Kim K anayetarajia mtoto wake wa kwanza na rapper Kanye West yupo Nigeria kwa ajili ya ku co-host concert iitwayo ‘Love Like A Movie” ya Darey Art Alade, itakayofanyika kesho tarehe 17 February huko Eko Hotel Convention Center.


Kim alitua airport akiwa na bodyguard wake pamoja na makeup artiste
Wakati huohuo Kim ameuza mjengo wake uliomgharimu dola milioni 4.8 aliununua mwaka 2010. Inasemekana ameuuza kwa chini ya bei hiyo pamoja na samani za ndani kama makochi. Mjengo aliouuza alikuwa akiutumia yeye na x-boy friend wake, Kris Humphrey! 




Nje mpaka ndani ya mjengo alioupiga bei KK

DRAKE AZUIWA KUINGIA CLUB SABABU YA CHRIS BROWN!


Chris Brown na Drake sasa hawapikiki chungu kimoja! Usiku wa Jumatano Drake alizuiwa kuingia club moja sababu Chris Brown alikuwa tayari ndani!

Mabaunsa waliokuwa mlangoni klabuni Playhouse huko Hollywood walimkatalia katakata Drake kuzama ndani kula bata na wanae vile CB alikuwa tayari akila bata na washkaji zake katika party ya kampuni ya mavazi ya ‘Popular Demand’.
 
Mabaunsa walijuafika kuwa kama Drake angeingia ndani basi pengine kingetokea kilekile kilichotoka W.i.P. nightclub. Unakikumbuka? Majamaa walitupiana vyupa sana na kusababisa uharibika wakutosha!

Ki-gentleman, Drake alisepa zake kimyakimya bila kubishi!


EXCLUSIVE: MAPYA YA MAREHEMU GOLDIE: MUME WAKE AIBUKA NA USHAHIDI KIBAO WA PICHA ZA HARUSI YAO!















EXCLUSIVE: MUME WA GOLDIE AIBUKA, AMPIGA BITI PREZZO!


Nobody knew bout this! Kumbe Goldie Harvey, mshiriki wa BBA stargame alikuwa ameolewa kabla hajafa! Andrew Harvey, raia wa Uingereza ameibuka na picha zote za harusi yao waliofunga kwa siri nyingine kibao wakati wakila bata pamoja.

Andrew na Goldie Harvey
Andrew na Goldie Harvey batani.
Andrew Harvey ameongeza kuwa yeye na Goldie walikuwa bado katika mahusiano na mawasiliano mazuri mpaka umauti ulipomfika. Andrew alikutana na Goldie katika party ya rafiki yake huko Lagos. Ndipo mfanyabiashara huyo wa mafuta akafunga ndoa na Goldie, December, 2005. Pia Andrew amekana marehemu Goldie kuhusishwa na matumizi yaliopitiliza ya madawa ya kulevya kuwa ndio moja ya sababu za kifo chake!


Upande mwingine pia Andrew Harvey alimpiga biti Prezzo na kumtaka kutojihusisha kabisa na maswala yoyote ya Goldie. Prezzo na Goldie walikuwa wakutane Lagos tarehe 15 February kwa ajili ya kusherehekea Valentine’s. 

Prezzo na Goldie mjengoni BBA