Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday, 29 January 2013

T.I ATOA MAONI JUU YA KUDHIBITI UMILIKI HOLELA WA SILAHA


President Barack Hussein Obama yupo katika mchakato wa kutengeneza sheria ya kidhibiti umiliki wa silaha. Papper T.I ana yake aliyoyasema katika interview na Larry King. ‘Larry King Now’. Check video ya interview hiyo!

CHRIS BROWN AZICHAPA STUDIO


Jana Jumatatu Rihanna’s boyfriend Chris Brown alizichapa kavukavu dhidi ya Christopher Francis Ocean better known on stage as Frank Ocean. Brown alikuwa studio akimsikiliza mmoja wa wasanii wake na alipotaka kusepa ndipo alipokutana na Ocean akiwa na kundi lake. Ocean na wanae walikuwa wanamzuia Brown asiondoke huku Ocean akimwambia Brown kuwa hii ni studio yangu na umepaki gari lako katika sehemu yangu. 

Brown akaona isiwe ishu akasogea ampe mkono Ocean, Mara mmoja wa kundi la Ocean akamvamia Brown. Hapo ndipo Brown nae akalianzisha akipewa sapoti na washkaji zake pia!
Brown Vs Ocean
Mpaka polisi walifika eneo la tukio lakini Brown alikuwa ashasepa na Ocean alipohojiwa alisema kuwa chanzo ugomvi wao ni Brown kupaki katika eneo lake na kwamba Brown amemchapa makonde. 
Frank Ocean's twitter account
Frank Ocean ni singer pia mwandishi na ameshawaandikia mastaa kama Brandy, Justin Bieber, and John Legend.  

50 CENT: RICK ROSS AME-FAKE AJALI YAKE


Hatimaye rapper 50 Cent ameibuka na kumkashifu Rick Ross kuwa amefeki ajali aliyopata jana asubuhi wakati akitokea kwenye birthday party yake ambapo akiwa njiani alirushiwa risasi hivyo gari lake, Royce Rolls, kuhama njia na kugonga nyumba. Cent aliandika katika akaunti yake ya twitter, “Hahahaaaaaa Bonge amegonga nyumba? Inaonekana ni ishu ya kufoji.................................”

'Hahaha fat boy hit the building? Lol it looks staged to me, I ride like OBAMA level 6 bulet proof bomb proof, you already know. [sic]'


Ingawa 50 ameonyesha ku-dought tukio hilo lakini picha zinaonyesha wazi matobo ya risasi katika matairi, bampa na taa za gari la Ross. Ross na 50 wana bifu la muda mrefu toka 2009 Ross alipomchana Cent katika ngoma yake Mafia Music.

Gari ya Ross
Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa katika gari alilokuwemo Ross, girlfriend wake Shateria L. Moragne na dereva wao. Japokuwa 50 ameonyesha mashaka lakini polisi wameichukulia ishu serious na bado wanaifanyia uchunguzi kwa sasa.

Ross
Ross, P Diddy, Fabolous Quincy Combs na Christina Milian

RICK ROSS ANUSURIKA KIFO


Alfajiri ya jana Jumatatu, The Miami based rapper William Roberts a.k,a Rick Ross alinusurika kuuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana. Ross alikuwa akitoka kwenye birthday party yake ya 37. Party hiyo ilihusisha list ndefu ya mastaa wakiwemo P Diddy, Fabolous Quincy Combs na Christina Milian just to mention a few.

Ross
Ross na Diddy
Ross, P Diddy, Fabolous Quincy Combs na Christina Milian
Rick Ross akiwa njiani huko Las Olas Boulevard baada ya kula bata usiku mzima, alianza kutupiwa risasi yeye akiwa ndani ya gari lake aina ya Rolls Royce ya silver isiyoingiza risasi! Katika sekeseke hilo dereva wa Ross alijikuta aligonga nyumba ya watu baada ya gari kupoteza mwelekeo.

 Hakuna mtu aliyejeruhiwa kutokana na taarifa ya polisi lakini inasemekana kuwa pengine bifu la muda mrefu lililopo kati yake na 50 Cent inaweza ikawa sababu.