Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday, 8 August 2012

HAPPY BELATED B-DAY TO NANCY SUMARI


Jana ilikuwa siku ambayo Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari, ambaye ni mshiriki pekee kutoka Tanzania kuwahi kufanya vizuri kwenye mashindano ya Miss World baada ya kutinga  hatua za mwisho na hata  kunyakulia taji la Miss World Africa.
Nancy aliamua kusherehekea siku yake hii ya kuzaliwa kwa style ya aina yake kwa kushirikiana na  mabalozi wenzake wa kampeni ya ‘Elimu yao Wajibu Wetu’ Faraja Nyalandu na Rebeca Gyumi kwa kulitembelea bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni.



Nancy akiwa na Mhe. January Makamba, Rebecca Gyumi na Faraja Nyalandu

Katika kampeni yao Nancy na wenzake wana kauli iitwayo
"Changia Tofali" ambapo kila mtanzania mwenye mapenzi mema na elimu nchini anaweza kuchangia kwa kutuma  ujumbe fupi wa SMS yenye maandishi CHANGIA TOFALI kwenda kwenye namba 15564, na utatozwa Tsh 250. Lengo la kampeni hii  ni kuchangia ujenzi wa hostel 30 ambazo zitawahudumia wanafunzi wa kike 1,504.

BARNABA'S NEW MANAGER

Kama wewe si mfuatiliaji wa burudani ya hapa nyumbani Tanzania then huna haja ya kutokumjua manager mpya wa artist wa chart-buster song ya "Magube Gube" aitwaye Hellen Kazimoto.
Well kama ulikuwa humjui ni kuwa licha ya umri wake mdogo Hellen aliwahi kupiga kazi mjengoni aka Clouds kama  Events/ Projects, Logistics coordinator ambayo aliifanya kwa mafanikio makubwa.
Hellen kwa sasa ndiye anaemsimamia Barnaba anaetamba na his new single called "Sijutii Kwa Niliyempata" kwenye kazi zake zote za kisanii.
Tanzania Top Model hooked up with her ili kujua nini kilichomfanya akaamua kupiga chini kazi mjengoni na kuamua kuingia kwenye issue uya umeneja.
"Kikubwa kilichonifanya kuingia kwenye issue hii ni kupanua wigo wangu  wa kipato na kiukweli kuna tofauti ya kufanya kazi as mwajiriwa na kufanya kazi wewe kama wewe, so to me kufanya kazi zangu binafsi kunanipa uhuru zaidi"-Hellen ambaye pia anafanya kazi na kampuni ya South of A iitwayo 30 + Events ambayo ni kampuni dada wa Another Privilege ambazo zinadeal na outdoor events/projects pamoja na Club Fusion ambazo ni new clubs nchini.
"Ninatamani kuona Tanzania ikiwa na the so called msanii si msanii jina bali mwenye kila kitu kinachotakiwa kumfanya kuitwa msanii, kama kuwa na his/her own label  kama kina R Kelly, gym yake mwenyewe na vingine vingi ambavyo naamini kwa nguvu za Mungu na ushirikiano wa wadau wenye uelewa mpana wa mziki hapa nchini nitafanikiwa kuitimiza ndoto hii"-added Hellen ambaye anatarajia kumsimamia Joh Makini kwa siku za usoni.

MANENO ATAMANI KUUNDWA KWA UMOJA WA MAMENEJA NCHINI

Alimmanage TID enzi hiizooo, kisha akammanage Diamond na baadae Sam wa Ukweli and recently jamaa kasitisha mkataba wa kufanya kazi na Rich Mavoko kabla ya kutimkia kwa crew mpya jijini ya Watanashati ambayo iko chini ya big boss himself aitwaye Uastaadhi Juma na Musoma.
   "Tatizo kubwa ambalo tunalo kwenye music industry is that msanii anaona yeye ni mjuaji zaidi kuliko manager and that the success anayopata ni kutokana na nguvu zake, which is very wrong. Imagine manager ndo anayempika msanii, anam-set katika njia ambayo anahisi ni rahisi kuuza kazi zake, anam-brand kama product ili aweze kumnadi kwenye market, anahangaika kumtafutia producers, sponsors, shows, deals, etc.. manager ndo ambaye anafikiria maslahi ya wasanii, anayaweka mbele hata kabla ya kwake mwenyewe. Iweje msanii anapofanikiwa kuitwa star na kuingiza shs mbili mfukoni anamdharau manager wake? mtu aliemtoa from the lowest?? hii mbayaaa"- Maneno.
   Anyways,  manager Maneno anadai kwamba haimsumbui kuhama from one artist to another infact it makes him proud kwamba Diamond is one of the leading bongo artist tulienaye na anatamani kumuona akifika mbali zaidi.
 ''Dhana ya kwamba mimi  najaribu kuwadidimiza wasanii ambao nimevunja nao mkataba si kweli, mimi nafurahia mafanikio yao,  tena natamani sana kuwatengeneza TID wengine kama sita hivi, na Diamond wengine kama watano hivi.. ili bongo flava izidi kukua"
" Tatizo  ni kwamba managers wa hapa Tanzania hatuna thamani kama ilivyo kwa wenzetu,  tunadharaulika sana.Kwanini tusiunde chama ambacho kitakua na sheria za kutulinda na kutuongoza? hii itatupa msimamo hata  kwa wasanii ambao tunawasaidia halafu baadae wanatuona si lolote, si chochote.." added Maneno.

SAMIR AKATAA KUJITOA KWENYA MKATABA WA RINGTONES

Msanii wa bongo fleva Samer Kassim aka Samir amekuwa msanii wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema  hawezi vunja mkataba na kampuni inayosimamia nyimbo zake kwenye ringtone sababu bado analipwa pesa nzuri sana na bado anafaidika sana na mauzo ya ringtone ya  wimbo wake wa kwanza  "Ukipenda" uliotoka mwaka 2009 kupitia Rocker Tz Recods uliotengenezwa na producer Tris , fahamu kuwa Wimbo huo ulimpa Samer show 53 Tanzania tu na kumtambulisha katika game la bongo fleva . 

Samir alisema anaamini wasanii wote waliovunja mkataba walijipanga kwanza na kuona hio ndio njia nzuri ya kuboresha mambo yao na yeye atakaa chini na wasimamizi wa kazi zake na kuona uamuzii wao.
Kwa sasa Samir tayari anatamba na ngoma yake mpya iitwayo  "Sina Raha"

Wednesday, 18 July 2012

FINA MANGO ATUA MAGIC FM


Baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kusikika redioni mashabiki wa Fina Mango wana uhakika wa kuanza kuisikia tena sauti yake tamu.

Mtangazaji huyo wa zamani wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, hatimaye  amehamia Magic FM.

Akiwa Magic FM, Fina Mango atakuwa akiendesha kipindi cha 'Mkutano' ambacho kitakuwa kikisikika kila  Jumamosi kuanzia saa 9.00 alasiri – 12 jioni.

Kipindi hicho kiitwacho ‘Makutano’ kitaruka kwa mara ya kwanza tarehe 4 mwezi ujao (August).
“My first radio crush is making a comeback…all the best @Fina_Mango cant wait to hear you again on air,” aliandika shabiki wake wa zamani aitwaye Lijocha.
Apparently, Fina Mango atafanya kipindi hicho kwa makubaliano maalum na sio kuajiriwa kwakuwa tayari ana kampuni yake iitwayo 1Plus Communications.