Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday 8 August 2012

HAPPY BELATED B-DAY TO NANCY SUMARI


Jana ilikuwa siku ambayo Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari, ambaye ni mshiriki pekee kutoka Tanzania kuwahi kufanya vizuri kwenye mashindano ya Miss World baada ya kutinga  hatua za mwisho na hata  kunyakulia taji la Miss World Africa.
Nancy aliamua kusherehekea siku yake hii ya kuzaliwa kwa style ya aina yake kwa kushirikiana na  mabalozi wenzake wa kampeni ya ‘Elimu yao Wajibu Wetu’ Faraja Nyalandu na Rebeca Gyumi kwa kulitembelea bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni.



Nancy akiwa na Mhe. January Makamba, Rebecca Gyumi na Faraja Nyalandu

Katika kampeni yao Nancy na wenzake wana kauli iitwayo
"Changia Tofali" ambapo kila mtanzania mwenye mapenzi mema na elimu nchini anaweza kuchangia kwa kutuma  ujumbe fupi wa SMS yenye maandishi CHANGIA TOFALI kwenda kwenye namba 15564, na utatozwa Tsh 250. Lengo la kampeni hii  ni kuchangia ujenzi wa hostel 30 ambazo zitawahudumia wanafunzi wa kike 1,504.

No comments:

Post a Comment