Ni muda sasa umepita tangu bifu la Bobi Wine na Bebe Cool lianze na sio kwamba linaelekea kufifia au kufa, la, bado mafahali hawa wawili hawaivi chungu kimoja! Na juzi tu Bobi Wine alikuwa na haya kumwambia Bebe Cool.
"Sina tatizo lolote na Bebe Cool lakini ana matatizo na yeye mwenyewe, ni kama vile watoto wadogo wakati mnakua. Wengine hukua na kupevuka haraka na wengine hubaki nyuma kama yeye ila sitaki anirudishe nyuma. Ni kama vile niliponunua ndege yangu, yeye hupenda kuzungumzia vitu vyangu kwa vile nam-inspire, inafurahisha sana"
Itabidi abadilishe ratiba yake upya kwa masaa 1,000 toka sasa baada ya mahakama ya huko Los Angeles kumhukumu Chris Brown kwa kufanya kazi za jamii. Hukumu hii inakuja baada ya Chris Brown kuonekana aliwasilisha ripoti ya uongo inayoonyehsa kuwa alitumikia kiukamilifu adhabu ya aliyopewa awali ya kuitimikia jamii kwa siku 180.
Kosa hili la kuwakilisha ripoti feki inatokana na adhabu aliyopewa baada ya kukutwa hatia ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna.
Kanda ya Ilala usiku wa kuamkia leo ilimtoa mlibwende atakaeiwakilisha kanda hiyo katika Miss Tanzania mwaka huu. Aliyekuwa Miss Ilala Dorice Mollel jana alivikwa taji la Red's Miss Ilala 2013, na kujichukulia kitita cha 1.5 milioni. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Alice Isaac (1 milioni) na wa tatu ni Clara Bayo (laki 7).
Mwana Muziki Machachari Rihanna haachi vituko kila kukicha na hiki ndicho kituko kipya
Shindano la kumsaka mlimbwende wa Ilala litafanyika siku ya ijumaa tarehe 16/08/03 kuanzia saa 2 za usiku katika ukumbi Mpya na wa kisasa katika jengo la GOLDEN TOWER
Katika kuelekea kilele cha shindano hilo jana usiku kulifanyika shindano la vipaji katika ukumbi wa city sport longe ambapo wasichana watano kati ya 10 walioshiriki shindano hilo walifanikiwa kutinga fainali ambapo fainali hzo zitaendana na sambamba na kumpata Redd;s Miss Ilala 2013.
Cheki picha mbali mbali za tukio hilo.