Kupitia internet biashara kwa wasanii huko
Naija imekuwa ngumu sana baada ya kujitokeza makundi ya watu kadhaa wakifanya
wao ni mapromota hivyo kuchukua advance za wasanii mbalimbali huku wasanii
wenyewe wakiwa hawajui lolote! Mwaka jana kuna
mtu alilamba dola 100,000/= kupitia twitter na facebook kwa kudai kuwa yeye ni
promota wa kundi la P-Square nchini Ufaransa.
P-Square wametoa onyo kwa wale watakaotaka kuingia nao mikataba
ya show kwa kuwa makini na watu hawa katika mitandao hii ya kijamii! Kupitia
akaunti yake ya twitter, Peter Okoye alitoa onyo kwa kuandika:
Kwa sasa P-Square ndio wasanii wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi nchini Nigeria kwa kuchaji dola 150,000/= kwa shows za kimataifa na Naila milioni 10 kwa shows za nyumbani kwao Nigeria!