Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday, 18 March 2013

SIKU YA 6: LIL WAYNE BADO HAJITAMBUI ICU!

Ni siku ya sita sasa toka Lil Wayne akimbizwe hospitali, L.A.'s Cedars-Sinai hospital akiwa hajitambui. Na bado mpaka sasa yupo ICU akiwa hajitambu. Ni kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya kupindukia. 

Mastaa wakiwemo Drake na Nicki Minaj, Eminem, Birdman na wengine kibao walimiminika hospitali kumjulia hali Wayne. Kitanda cha Lil Wayne kimezungukwa na ndugu jamaa na marafiki wakimwombea afya njema na vilio vimetawala pia hospitalini hapa!

 
Madaktari wanaomtibia Wayne ilibidi wali-flash tumbo lake mara 3 ili kuondoa madawa ya kulevya aina ya 'codeine' baada ya Lil Wayne kubugia madawa hayo kupitiliza!

















P-SQUARE WAISIMAMISHA MALAWI!

The Alingo stars, P-Square wako katika tour yao katika mataifa ya barani Afrika na wik-end iliyokwisha walikuwa nchini Malawi na kuangusha bonge moja la show. Show ilikuwa hivi:








JUMBA BEI GHALI ZAIDI NCHINI UINGEREZA!

Hii ndio nyumba ghali nchini Uingereza. Kutokana na bei yake kuwa juu sana ilibidi ipunguzwe kwa takribani pauni milioni 35. Na hii imechukua miaka miwili bila mnunuzi kupatikana.  Na sasa bei yake ni pauni milioni 65 tu!


Bangaloo hili lina vyumba 14 vya kulala na linapatikana katika mtaa wa Hampstead, mtaa huu unajulikana kama 'Billionaires' row' kwa sababu wakazi wa eneo hilo ni wanauwezo kiuchumi!



 Jumba hili la kifahari lilijengwa mwaka 1910 liliwekwa sokoni toka mwaka 2011 na bei yake ilikuwa ni pauni za Uingereza, milioni 100.






















Sunday, 17 March 2013

PETER MSECHU KUZALIWA UPYA KESHO!

Peter Msechu kesho atasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka kadhaa. Peter Msechu ambaye ni Bongo Star Search na Tusker Project Fame Star anatarajia pia ku-release his new hit single hiyo kesho. 

Ngoma hiyo inaitwa 'Kumbe' amemshirikisha 'Mwamba wa Kaskazini', Joh Makin!   

Happy Birthday Peter Msechu.




Saturday, 16 March 2013

ALINGO Vs AZONTO

Kumeibuka ghasia na kutupiana kwa maneno katika mitandao ya jamii baina ya Wanigeria na Waghana kuhusiana na styles hizi mbili za Alingo na Azonto. Na sokomoko hili limekuja hasa baada ya artiste wa dancehall toka Ghana, Samini kutoa ngoma kwa kutumia biti ya Alingo kuwadis P-Squae kwa kukopi dance ya Azonto na kuitumia katika Alingo!

 Wewe unafikiri style ipi ya ku-dance ni kali kati ya ile ya Azonto na Alingo? Na je, ni kweli styles hizi zinafanana?