Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday, 19 January 2013

CHRIS BROWN NA RIHANNA JIKONI!

They are back! Not in love this time but kikazi zaidi.  Hii itakuwa collabo yao ya nne kwa Chris Brizzy na Rihanna ambao wameonekana wakitoka studio kurekodi pamoja. Mwaka jana Chris na Riri waliitingisha dunia kwa kufanya remixes ya ngoma zao, Birthday Cake na Turn Up the Music. 

Brown na Riri walioanza mapenzi yao mwaka 2008, walifanya collabo ya kwanza katika ngoma ya Umbrella ambayo Brizzy aliita Cinderella!

Ingawa bado haijajulikana ngoma hiyo itakuwa katika album ipi Rihanna bado ana shauku ya kuujulisha ulimwengu kuwa sasa Chris Brown is back in her life! The talk that talk ni kuwa Riri ameachia kipande cha ngona yake "Stay" katika akaunti yake ya Instagram yenye maneno, "Not really sure how to feel about it, Something in the way you move, Makes me feel like I can’t live without you. Funny you’re the broken one but I’m the only one who needed saving."

Kazi na dawa! Baada ya kurekodi ngoma, Brown na Rihanna waliibuka Emerson nightclub, Hollywood na baada ya kuparty pamoja, Rihanna alionekana akizama mjengoni mwa Chris Brown for a night cap!




































                      Brown na Rihanna wakitoka studio


 Rihanna akizama mjengoni mwa Brizzy

                               "Nobody's Business"









JUSTIN BIERBER ASHINDA KESI!

Justin Bieber ameibuka kidedea dhidi ya mwanamke mmoja aliyemfungulia kesi ambayo Bieber alitakiwa kumlipa bi-mkubwa huyo dola milioni 9.

Mwanamama huyo alifungua kesi akimlalamikia Bieber kupasuliwa ngoma za masikio yake kwa mziki mzito na makelele ya nyomi la watu waliohudhuria concert ya Bierber iliyofanyika mwaka 2010. Mama huyo aitwaye Stacey alihitaji fidia ya dola milioni 9 lakini cha kushangaza, wiki iliyopita aliiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo. 

Sababu ya kuiomba mahakama kuiweka kapuni kesi hiyo, Stacey alisema kuwa hana wakili hivyo kuendelea na kesi hiyo haitowezekana ingawa bado anaamini angeweza kushinda kesi hiyo.

  JB



Friday, 18 January 2013

KENYA'S RICHEST FEMALE CELEBRITY; SIZE 8 OR THE DRUMMER QUEEN?


Kufuatia taarifa zinazoifunika Kenya's music industry kuwa Size 8 ndio the richest celebrity kutokana na endorsements kadhaa na makampuni makubwa kama kampuni ya mtandao wa simu Safaricom na Royal Media Services na kumfanya aingize mkwanja mrefu katika bank accounts zake huko Kenya.

However, mtazamo huo umepingwa vikali na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya burudani na kum-crown "Mikono kwenye Hewa" singer Muthoni the Drummer Queen kama ndiye the female artist anayekamata mpunga mnono zaidi ya duu yeyote. Hii imetokana na calculations zilizofanywa kutoka katika biashara anayofanya The Drummer Queen ya "Blankets and Wine".

Mahesabu yaliyofanywa fastafasta tu Muthoni the Drummer Queen anakadiriwa kulamba mpaka 15 Million Kenyan Shillings Per Month. 

There is absolutely NO OTHER female celeb with a cashflow source like that in Kenya. Hata huyo Size 8 hakamati hapo.

Muthoni The Drummer Queen

 Size 8
 

"FOR GIRLS ONLY"

Peter Okoye one half of P-Square hivi majuzi alipost picha hizo hapo chini katika ukurasa wake wa Instagram with the above heading as a caption.

Is he trying to attract beautiful ladies out there with his "six packs"?

  Do you feel him girls out there?


                            Take yo shirt off!

                            Like Fally Ipupa like Peter Okoye!

   With his Lamborghini Gallardo worth USD 200,000

EXCLUSIVE: BILIONEA NO.1 AFRICA ANUNUA BOTI YA KIFAHARI!

Aliko Dangote, bilionea namba moja Africa kutokana na takwimu za Forbes Magazine akikadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 12, juzi tarehe 17 alifanya kufuru ya kununua boti ya kifahari na kuipa jina la "Mariya"

Chairman huyo wa Dangote Group of companies amefanya kununua just the same yatch na ile ya mpinzani wake Femi Otedola kukiwa na utofauti mdogo sana.

    Tabasamu la fwedha, Mzee Dangote.

    Boti la Aliko Dangote.