Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday, 5 January 2013

AMBER ROSE KUSHEREHEKEA KUWA MAMA

Amber Rose ambaye ni Mchumba wa Wiz Khalifa aonyesha wazi tumbo lake kwa kuvaa mavazi ya kubana akiwa na Chriss Brown pamoja na mchumba wake Wiz Khalifa.

Akiwa katika mavazi yake ya rangi ya njano mwanadada huyo ambaye ana umri wa miaka 29 hakuacha kutabasamu muda wote huku akipiga picha kuonyesha tumbo lake la ujauzito akiwa ni mama mtarajiwa.

Amber Rose Akipiga picha kwa tabasamu.

Amber Rose, Chriss Brown na Wiz Khalifa wakipiga picha wote wakiwa katika hali ya furaha

MARIO BALOTELLI AMWAGWA

Mshambuliaji wa timu ya Manchester City Mario Balotelli aachwa na Mpenzi 
wake Tabby Brown ambao wamedumu kwa muda wa miezi saba tu na kuingia mikononi mwa Msanii wa R&B Trey Songz. Mwanadada huyo alidai kuwa amechoshwa na kutoeleweka kwa mpenzi wake huyo Mario Balotelli na kuamua kuondokana na adha hiyo kwa kumtema.



                                         MARIO BALOTELLI                TABBY BROWN

TREY SONGZ

Friday, 4 January 2013

AGUERO NA MKEWE GIANNINA DIEGO MARADONA KWISHA KAZI

Aguero atengana na Mkewe ambaye ni mtoto wa gwiji la soka Argentina Diego Maradona aitwae Giannina baada ya uhusiano wao kwa muda wa miaka minne. Mkewe kwa sasa inaaminika kuwa anaishi Mjini Madrid pamoja na mtoto wao wa kiume aitwae Benjamin mwenye umri wa miaka mitatu.
Moja ya wapambe aliandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuonyesha kumponda Sergio Arguero (mchezaji wa manchester city) kwa kusema "Sergio Arguero hakufai kabisa kwani ni mshenzi na mpumbavu" lakini mwanamama huyo hakuridhika na maneno yaliyoandikwa na mpambe huyo na kumjibu kwa kifupi kuwa "usiseme hivyo kwani huyo ni baba wa mtoto wangu na hayuko kama wewe unavyofikiria"


RIri NA CHRISS MAMBO SAFI

Nani kasema mapenzi yamekwisha? Hata kama ukinitoa manundu nakupenda tu

Chriss Brown amgharamikia Rihana kwaajili ya kuenjoy X-mass na Mwaka mpya mapenzi motomoto
 wakiwa kwenye Basket ball siku ya X-Mass.

Mzee mzima Chriss uhakika mtupu hapo.

wakitoka nje  ya duka la Slurpee baada ya shoping.

RICK ROSS ALIVYOWARUSHA WATU MKESHA WA MWAKA MPYA


Rick Rozay akiwarusha mashabiki wake katika mkesha wa mwaka mpya katika visiwa vya Bahamas.