Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 6 September 2012

KITALE AJA NA SIMU YA KICHINA


Musician na pia comedian naekuja kwa kasi nchini kwa jina la Kitale ameungana na Kampuni ya Bau Entatainment ya jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa filamu ijulikanayo kama 'Simu ya Kichina'.

Ndani ya filamu hiyo Kitale ameshirikiana na wenzake toka kwenye tasnia ya Bongo movie ambao ni pamoja na Kitale mwenyewe,  Ringo,Kingwendu na Mtanga.
"Ndani ya filamu hii kuna mafundisho kibaoambayo ni pamoja na ugumu wa maisha ambao unaweza kumpa mtu changamoto ya maisha ambayo yanaweza kukuletea maendeleo,vilevile ugumu wa maisha waweza sababisha tamaa ambayo yaweza kupelekea kuwa mwizi katika maisha yako na kukusababishia maisha yako kuwa magumu", Kitale.

Filamu hiyo kwa sasa ipo mtaani kwa ajili ya kuwapa wapenzi mbalimbali burudani wakiwa majumbani kwao.
Dont miss it....'Simu ya Kichina' is a must watch movie.

OFFICIAL DJ WA CHRIS BROWN KUWASHA MOTO JUMAMOSI HII JIJINI DAR




Party people mko tayari.
Sikia hii G5 Click kwa kushirikiana na Richboys Entertainment watamdondosha kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya Tanzania DJ Babey Drew toka America kuja ku-spin kwenye party itakayoitwa Tipsy Night on 8 September 2012 ndani ya Savannah Lounger iliyoko Quality Center.
Kama ulikuwa hujui ni kuwa DJ Babey Drew ni official dj wa Chris Brown.

PICHA ZA DIAMOND ALIPOKUWA MAREKANI KWENYE SHOW



AY BALOZI MPYA WA AIRTEL NCHINI

AY(kushoto), Jackson Mmbando (meneja mahusiano at Airtel) na Hawa Bayuni (meneja huduma wa Airtel)


Ambwene Yessaya aka AY ambaye kwa sasa anahit kwenye TVs na radio airwaves with his song called  "Party Zone" amakamata dili la kuwa balozi mpya wa mtandao wa Airtel nchini akimrithi Ally Kiba aliyekuwa balozi wake msimu uliopita.
"Tumeamua kumpa dili hili AY baada ya kuvutiwa na kazi zake kwa ujumla, amekuwa msanii mwenye tunzo nyingi za kitaifa na pia kimataifa achilia mbali collabos ambazo amekuwa akizifanya na wanamuziki wa kimataifa bila kusahau shows ambazo amelkuwa akizifanya kwney majukwaa mbalimbali ya kimataifa", Jackson Mmbando ambaye ni manager mahusianao wa matandao huo.
Kwa kuanzia, AY alisema atafanyia kazi mradi wa kuchangia elimu ambao Airtel
 inashirikiana na BAMVITA.
"Nawaomba  Watanzania kuchangia mradi huo kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 ambapo watakatwa shilingi 200 katika mradi huu au wengine kuchangia kwa Airtel Money kupitia namba 0788 041361", AY ambaye pia alikabidhiwa simu aina ya Samsung Galaxy Tab7.0 Plus yenye thamani ya Sh. 1.200,000
 na Mmbando, sambamba huduma zote ambazo zinalipiwa na Airtel.

VIDEO YA BAADAE YA OMMY DIMPOZ KUZINDULIWA JUMAPILI HII MAISHANI



Singer wa "Nai Nai" na "Baadaye" na mshindi wa tunzo mbili za Kili Music Award 2012, Ommy Dimpoz anataraji kuzindua video yake mpya ya "Baadaye" at the   New Club Maisha jumapili hii.
“Kazi hii ambayo tutaizindua jumapili hii pale Maishani ni ya uhakika kila atakayeiona ata-appreciate" alisema Mubenga ambaye ni manager wa Ommy Dimpoz.
Uzinduzi wa video hiyo ambayo imefanyika huko South Africa chini ya director Adam Juma wa Visual Lab utasindikizwa na wasanii kama  Chegge Chigunda, Suma Mnazareth na Nas 3.