Zoezi la kwasaka watu watakaoweza kuingia kwenye shindano la Maisha Plus, imeanza jana (Agosti 27) huko Bagamoyo mkoani Pwani...
Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo;
Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu
Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe
Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro
Usaili utafanyika Karatu
Agosti 31 – Singida
Usaili utafanyika Singida Mjini
Septemba 1- Iramba
Usaili utafanyika Iramba Mjini
Septemba 2- Dodoma
Usaili utafanyika Kondoa Mjini
Tanzania top model audition
Tanzania top model audition
Tuesday, 28 August 2012
Monday, 27 August 2012
KANYE AMFANYA KIM K KUBADILI NGUO ZAKE ZOTE
Kanye West anamtaka mpenzi wake Kim Kardashian avae mavazi ya heshima na ya kuvutia.
Katika kipindi cha jana cha Keeping Up With the Kardashians,
rapper na mbunifu huyo wa mavazi, 35 – ameweka deal na mpenzi wake huyo wa
miezi mitano kuwa kama atazitupa nguo zake zote atamnunulia zingine.
BBC DIRA YA DUNIA KURUKA LIVE LEO KWENYE TV
![]() |
| Saleem Kikeke |
Matangazo ya televisheni ya Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili
ya BBC leo yanaanza kuruka rasmi kupitia Star TV ya Tanzania na Qtv ya Kenya.
Wiki iliyopita kulifanyika uzinduzi wa matangazo hayo jijini Dar es Salaam.
Matangazo hayo ya Dira ya Dunia kwa upande wa radio ni maarufu
zaidi pengine kuliko matangazo yote ya radio za kimataifa zinazotangaza
Kiswahili duniani.
Kuingia kwenye matangazo ya runinga kwa BBC Swahili kunafungua
ukurasa mpya wa matangazo ya aina hiyo ya Kiswahili nchini.
BBC Dira ya Dunia siku za usoni itakuwa ikishindana na matangazo mengine
ya Kiswahili ya Al-Jazeera ambayo yapo kwenye mchakato wa kuanzishwa.
CHIWAWA WA KENYA AZINDUA MAJI YAKE
Rapper wa Kenya aliyewahi kutamba na ngoma kali iitwayo ‘Mnafeel
aje’, Chiwawa amezindua maji yake ya kunywa.
Maji hayo yanaitwa Minerva jina la kigiriki la mungu wa
busara aliyekuwa akihusishwa na maji katika sehemu ya story zake.
Kwa upande wa Tanzania, Lady Jaydee aliwahi kujaribu
kuanzisha maji yake lakini hata hivyo hayakuendelea kutolewa kutokana na sababu
ambazo hazikuwekwa wazi.
Subscribe to:
Posts (Atom)



