Mtupa makonde mashuhuri Ulimwenguni, Mike 'Iron' Tyson yupo katika hali mbaya kiafya. Hayo ameyatamka yeye mwenyewe akiwa katika shughuli ya ku-promote ESPN's Friday Night Fights huko Turning Stone Resort, New York Ijumaa iliyopita. Tyson alikaririwa akisema, "Wakati mwingine mimi ni mtu mbaya, nimefanya vitu vingi vibaya na nahitaji kusamehewa. nahitaji kubadilika. nataka kuishi maisha mazuri nikiwa timamu. Sitaji kufa, vile kwasasa niko hatarini kufa kwasababu siwezi ishi bila kutumia madawa ya kulevya au kilevi kikali chochote". Mike Tyson alikwenda rehab mara tatu na angalau sasa hivi anaanza kuonyesha matumaini ya kupona toka katika matumizi ya madawa ya kulevya!
Katika party ya Budweiser-America Music festival iliyofanyika wikiend hii huko Philadelphia, Pennsylvania mwanamama Amber Rose alichora tattoo ya msalaba uliogeuzwa kichwa chini miguu juu katika paji la uso wake huku akivuta sigara! Hii ni show ambayo mume wake Wiz Khalifa alipanda jukwaani kupiga show! Alama hii inahusishwa na waabudu Shetani!
Wakati show za utoaji tuzo za Channel O zikitarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 30 November huko Walter Sisulu Square, Kliptown Soweto, msanii AY pekee toka Tanzania ndiye aliyeweza walau kuingiza video yake moja ya "Paty Zone" katika categories mbili tofauti, ambazo ni "Most Gifted Male Video" na Most Gifted African East Video", video ambayo imetengenezwa Afrika Kusini na Godfather. Wakati huohuo jirani zetu Wakenya wameingiza videos 8 katika categories tofauti tofauti!
Wapo Xtatic/Aka & Priddy Ugly, STL, Sauti Sol, P-Unit na P-Unit! Toka Uganda, Radio na Weasal pekee ndio wamewakilisha. Pengine hii ndio sababu ya baadhi ya wasanii wa Bongo kukimbilia Kenya ili kupata kilicho bora katika videos zao! Nigeria ndio nchi iliotoa wasanii wengi kuliko nchi yoyote Afrika, wameingia katika categories 20!
Picha tofauti za Miley Cyprus na Robbin Thicke katika jukwaa la Video Music Awards (VMA2013). Chini kulia ni familia ya Will Smith wakishangaa wasiamini kinachotokea jukwaani!