Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Monday, 9 September 2013

AMBER ROSE NA TATTOO YA MSALABA ULIOGEUZWA!

Katika party ya  Budweiser-America Music festival  iliyofanyika wikiend hii huko Philadelphia, Pennsylvania mwanamama Amber Rose alichora tattoo ya msalaba uliogeuzwa kichwa chini miguu juu katika paji la uso wake huku akivuta sigara! 

Hii ni show ambayo mume wake Wiz Khalifa alipanda jukwaani kupiga show! Alama hii inahusishwa na waabudu Shetani!



WAKENYA WAONGOZA AFRIKA MASHARIKI CHANNEL O

Wakati show za utoaji tuzo za Channel O zikitarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe  30 November huko Walter Sisulu Square, Kliptown Soweto, msanii AY pekee toka Tanzania ndiye aliyeweza walau kuingiza video yake moja ya "Paty Zone" katika categories mbili tofauti, ambazo ni "Most Gifted Male Video" na Most Gifted African East Video", video ambayo imetengenezwa Afrika Kusini na Godfather. Wakati huohuo jirani zetu Wakenya wameingiza videos 8 katika categories tofauti tofauti! 


Wapo Xtatic/Aka & Priddy Ugly, STL, Sauti Sol, P-Unit na P-Unit! Toka Uganda, Radio na Weasal pekee ndio wamewakilisha. Pengine hii ndio sababu ya baadhi ya wasanii wa Bongo kukimbilia Kenya ili kupata kilicho bora katika videos zao!

Nigeria ndio nchi iliotoa wasanii wengi kuliko nchi yoyote Afrika, wameingia katika categories 20!


Monday, 26 August 2013

SHOW YA UCHI YA MILEY CYPRUS KATIKA VMA 2013

Picha tofauti za Miley Cyprus na Robbin Thicke katika jukwaa la Video Music Awards (VMA2013). Chini kulia ni familia ya Will Smith wakishangaa wasiamini kinachotokea jukwaani!

Friday, 23 August 2013

SKETI YAMVUKA TONI BRAXTON STEJINI!

Mwanzomi mwa wiki hii huko New Jersey, mama wa watoto wawili, mwanamuziki Toni Braxton aliwapa mashabiki wake zaidi ya kile walichokilipia kwaajili ya show hiyo. Wakati akiwa stejini akipiga show hiyo Toni Braxton, 42, alishangaa akiona sketi yake nyepesi ya metallic akimvuka na kuacha makalio yake wazi!




Kwa bahati mbaya Toni Braxton hakugundua kuwa sketi yake imemvuka kwani aligeuka na kuwapa mashabiki mgongo huku akitingisha makalio yake kwa mbwembwe asijue kinachoendelea kumbe ndio anawamwagia utamu huku mashabiki wakilipuka kwa shangwe la hatari!



Toni Braxton aliendelea na show mpaka jamaa mmoja alipokwea stejini na kumfunika kwa koti la suti yake.



Thursday, 22 August 2013

DIAMOND KULA MKWANJA MREFU KWA KUFANYA COLLABO KENYA

Mshindi wa tuzo ya mwimbaji bora wa Gospel nchini Kenya, Willy Paul ametangaza kupiga kolabo na msanii mwenye kukamata headlines kila uchao Bongo na nje ya Tanzania, Diamond Platinumz! Willy alikutana na Diamond katika concert moja iliyohappen huko Nairobi Ijumaa iliyopita.

"Diamond alivutiwa sana na kazi zangu kama mimi kwa kazi zake. Nafahamu anachaji pesa so nitamsikiliza anahitaji kiasi gani na nipo radhi kumpa mkwanja autakao". 


.