Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Thursday, 22 August 2013

STAR WA PRISON BREAK AJITANGAZA NI SHOGA!

Starring wa tamthiliya ya Prison Break, Wentworth Miller a.k.a Michael Scofield ametangaza jana Jumatano kuwa yeye ni shoga. Amefanya uamuzi huu baada ya kukataa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za jumuiya ya wanafilamu katika mchakato wa kukataa au kupinga 'ushoga' nchinu Urusi.


Baada ya Michael Scofield kupokea mwaliko huo uliopewa jina la St. Petersburg International Film Festival, alisema, "Mimi kama shoga ni lazima nikatae". Scofield aliendelea kusema, "Nachukizwa na vile jinsi mashoga na wasagaji wanavyochukuliwa na serikali ya Urusi. Kwahivyo siwezi kushiriki katika kampeni hii ambapo watu kama mimi hawapewi haki zao za msingi"


Tuesday, 20 August 2013

BOBI WINE AMCHANA BEBE COOL!


Ni muda sasa umepita tangu bifu la Bobi Wine na Bebe Cool lianze na sio kwamba linaelekea kufifia au kufa, la, bado mafahali hawa wawili hawaivi chungu kimoja! Na juzi tu Bobi Wine alikuwa na haya kumwambia Bebe Cool.
 

"Sina tatizo lolote na Bebe Cool lakini ana matatizo na yeye mwenyewe, ni kama vile watoto wadogo wakati mnakua. Wengine hukua na kupevuka haraka na wengine hubaki nyuma kama yeye ila sitaki anirudishe nyuma. Ni kama vile niliponunua ndege yangu, yeye hupenda kuzungumzia vitu vyangu kwa vile nam-inspire, inafurahisha sana"







 

Saturday, 17 August 2013

CHRIS BROWN ATUPWA JELA

Itabidi abadilishe ratiba yake upya kwa masaa 1,000 toka sasa baada ya mahakama ya huko Los Angeles kumhukumu Chris Brown kwa kufanya kazi za jamii. Hukumu hii inakuja baada ya Chris Brown kuonekana aliwasilisha ripoti ya uongo inayoonyehsa kuwa alitumikia kiukamilifu adhabu ya aliyopewa awali ya kuitimikia jamii kwa siku 180.

Kosa hili la kuwakilisha ripoti feki inatokana na adhabu aliyopewa baada ya kukutwa hatia ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna.


DORICE MOLLEL NDIYE RED'S MISS ILALA 2013

Kanda ya Ilala usiku wa kuamkia leo ilimtoa mlibwende atakaeiwakilisha kanda hiyo katika Miss Tanzania mwaka huu. Aliyekuwa Miss Ilala Dorice Mollel jana alivikwa taji la Red's Miss Ilala 2013, na kujichukulia kitita cha 1.5 milioni. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Alice Isaac (1 milioni) na wa tatu ni Clara Bayo (laki 7). 


Thursday, 15 August 2013

RIHANNA TENA

Mwana Muziki Machachari Rihanna haachi vituko kila kukicha na hiki ndicho kituko kipya