Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Saturday, 13 April 2013

PAUL WA P-SQUARE APATA MTOTO!

Baada ya pacha wake Peter kupata mtoto wa pili wa kike sasa ni zamu ya Paul. Jana Paul Okoye na mchumba wake wa muda mrefu Anita, walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume. Mtoto huyo aliyepewa jina la Andre alizaliwa Atlanta, USA.

Peter tayari ana watoto wawili, toka kwa demu wake wa muda mrefu Lola Omotayo. Welcome to the world Andre Okoye.




SIZE 8: KUKAA UCHI BASI!

Baada ya msanii wa kike Size 8 kutangaza jana kuokoka, sababu ya haraka haikujulikana mapaka alipofanya interview na kutoa yale yaliokuwa yanamsibu. Size 8 ambae kuna wakati nchini Kenya alitangazwa kama msanii mwenye mkwanja mrefu kuliko wote alisema kuwa moja kati ya sababu za yeye kuokoka na kuacha mziki wa kidunia ni pale alipokuwa akitoka kupiga shows za usiku huwa analia usiku mzima na moyoni hakuwa akijisikia amani.


Pia Size 8 alisema kuwa kufuatia hali hiyo ya kutosikia amani moyoni mwake aliamua hata kuipiga chini show ambayo ilikuwa imuingizie milioni 2 za Kenya. Alipoulizwa kama ataendelea kuvaa vimini-vichupi na vinguo vifupi alivyokuwa akitupia hapo awali, Size 8 alisema, "hizo sasa zimekuwa mbaya. No more! No more skimpy clothing! Unajua hizo mavazi zinatisha watu. Sasa nitakuwa nikivaa mavazi za heshima. Mavazi zenye Jehovah pia anafurahia akiniona nazo. Si lazima ikuwe dress refu. Nguo tu ya heshima."


Size 8 tayari ameshatoa ngoma ya gospel iitwayo 'Mateke', icheki hapa:-



P-SQUARE WATOA ONYO!

Kupitia internet biashara kwa wasanii huko Naija imekuwa ngumu sana baada ya kujitokeza makundi ya watu kadhaa wakifanya wao ni mapromota hivyo kuchukua advance za wasanii mbalimbali huku wasanii wenyewe wakiwa hawajui lolote! Mwaka jana kuna mtu alilamba dola 100,000/= kupitia twitter na facebook kwa kudai kuwa yeye ni promota wa kundi la P-Square nchini Ufaransa.

P-Square wametoa onyo kwa wale watakaotaka kuingia nao mikataba ya show kwa kuwa makini na watu hawa katika mitandao hii ya kijamii! Kupitia akaunti yake ya twitter, Peter Okoye alitoa onyo kwa kuandika:
  

Kwa sasa P-Square ndio wasanii wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi nchini Nigeria kwa kuchaji dola 150,000/= kwa shows za kimataifa na Naila milioni 10 kwa shows za nyumbani kwao Nigeria!


Friday, 12 April 2013

AKON AMPONGEZA KENYATTA, AKOSOLEWA!

Baada ya kuapishwa na kuwa raisi kamili, pongezi mbalimbali zimekuwa zikitolewa na mmoja wa watu maarufu ambao hawakuwa nyuma kusifia jinsi mchakato mzima wa uchaguzi ulivyokwenda kwa amani na utulivu mpaka kupatikana kwa raisi Uhuru Kenyatta ni Akon. Baada ya hapo sasa zikatoka comments mbalimbali katika fanpage yake ambazo Akon alizipotezea lakini hii hakuiacha iende hivihivi.


Mmoja wa commenters aliandika hivi, "Huyu (Kenyatta) ni mwizi kama baba yake. Aliiba ardhi na kabila lake tu ndilo lililompigia kura. Kwa sasa ana kesi katika mahakama ya kimataifa na naamini watamtia hatiani. Kwanini (Akon) umpongeze?????"

Ndipo Akon akajibu, "Ndio maana Africa haiwezi kusonga mbele. Tunapoteza muda mwingi katika vitu visivyo na maana. Nimempongeza kwa kufanya uchaguzi kwa njia ya amani! Hii ni hatua kubwa kwa Afrika. Kama kuna lolote baya alilolifanya hapo nyuma ni yeye (Kenyatta) ataenda kujibu kwa Mungu. Sasa kwa kwanini ujiumize kichwa? Sisi sio watu wa kumjaji!"




REEBOK WAMTEMA RICK ROSS BAADA YA KUBAKA!

Hatimaye kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo Reebok imemtema rasmi Rick Ross. Hii ni baada ya the Maybach Music rapper The Boss kutema lines zenye utata tena zenye kumzalilisha mwanamke na kuonekana kama alibaka mwanamke kwa mistari yake katika ngoma ya "U.O.E.N.O".

Mistari ya Rossay inasomeka, ‘Put molly all in her champagne, she ain’t even know it/I took her home and I enjoyed that, she ain’t even know it’. Akimaanisha anamuwekea molly (kilevi) kwenye kinywaji/shampeni ya demu bila yeye kujua. Anampeleka nyumbani kwake na kum-do bila yeye (demu) kujua.
Wanaharakati waliowahi kubakwa juzi kati waliandamana mpaka ofisi za Reebok kuwaomba waache kumdhamini Rossay na Reebok leo hii wametoa tamko kuachana rasmi na rapper huyo na kusikitishwa kwa kile Rossay alichokifanya katikam ngoma hiyo ya Rocko.