Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Tuesday, 12 March 2013

B.I.G ARUDI DUNIANI!


Ni miaka 16 sasa toka rapper notorious B.I.G auwawe kwa risasi huko Los Angeles, California. Siku 2 kabla ya kutimiza miaka hiyo 16 watoto wake B.I.G wametangaza kutoa movie inayoitwa House of Wallace, itakayowahusu wao na baba yao B.I.G katika mfumo wa katuni!

Watoto wa B.I.G, C.J. Wallace, 16 na T'yanna Wallace, 19 ndio mastaa katika movie hiyo itakayo rekodiwa katika studio ya baba yao BIG, Brooklyn, New York, studio. 


C.J. Wallace
B.I.G a.k.a Christopher Wallace, ataonekana katika video hiyo kama mzuka hivi unaowapa mwongozo watoto wake juu ya studio yao, Brooklyn studio isichukuliwe na makampuni mengine makubwa yaliokuwa tayari kuinunua.
BIG atakumbukwa kwa ngoma zake kali kama ‘Mo money Mo Problems’ na pia ni kati ya waanzilishi wa East Coast hip hop scene miaka ya 1990

P.Diiddy never miss ishu yoyote inayomhusu mwanae B.I.G

CHRIS BROWN AVUTA BANGI STEJINI GHANA

Polisi nchini Ghana wameanza uchunguzi unaohusisha tukio la uvutaji wa bangi hadharani uliofanywa na rnb singer Chris Brown alipokuwa on stage kwenye show yake March 5, Accra Sports Stadium. Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi wakiwemo Waziri Mkuu wa nchi hiyo, wabunge kadhaa na Askofu Mkuu Charles Palmer-Buckle. 

Lakini waandaaji wa concert hiyo, Charter House wamepinga vikali tuhuma hizo kwa kusema kuwa 'Don't Wake Me Up' singer & Rihanna's boo alivuta 'cigar' na sio ganja kama watu wanavyodai.

Chris Brown stejini akifanya yake

Taarifa rasmi kutoka katika Idara ya Usalama Ghana zinasema kuwa wamepokea malalamiko kutoka makundi mbalimbali ya jamii na tayari uchunguzi wa tukio umeanza!
 

PAPA KUPATIKANA MIONGONI MWA HAWA!


Makardinali 115 waliokusanyika Vatican wakiimba litania ya watakatifu wote kabla ya kuanza rasmi mchakato wa kumchagua Papa mpya leo hii!

Monday, 11 March 2013

MARIAH CAREY IS BACK TO THE GAME!

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa Mariah Carey alifokas zaidi kulea watoto wake na pia kuwa jaji katika shindano la American Idol! Na sasa the diva herself is back to the business to the fullest! Mtoko mpya unaitwa 'Almost Home'. Ngoma hii pia imetumika kama soundtruck ya movie mpya, 'Wizard Of Oz'.


Albam ya mwisho ya Mariah ni 'Memoirs Of An Imperfect Angel' na ilitoka mwaka 2009. Carey, 42,  amekuwa bize sana kwa mazoezi na shughuli nzima ya kurekodi albam hii! 



Mariah Carey ameshaachia baadhi ya vipande (picha) vya ngoma hiyo na vinapatika hapa tu kwa sasa!


 


JUSTIN BIEBER AFUTA SHOW URENO!

Ni kama vile Justin Bieber amesanukia mchongo hivi na fasta kwa kushirikiana na waandaaji wa show yake wakaamua kuifutilia mbali show yake. Show ilikuwa ipigwe huko Ureno. Kimsingi JB alikuwa agonge shows mbili, moja tarehe 11 na nyingine tarehe 12 March. Sasa ya tarehe 12 ndio iliyopigwa chini na raia wote walionunua tiketi za show hiyo watarudishiwa mkwanja wao!


Habari toka katika mtandao wa ukumbi aliotakiwa JB kupiga show zinasema kuwa ni sababu za kibiashara zaidi ndio zilizofanya kufutwa kwa show hiyo.  Inasemekana Justin Bieber anahofia kupigia show viti kutokana na yale yaliyotokea katika concert yake huko London ambako alichelewa kwa zaidi ya dakika 45 na kuwaudhi mashabiki wake hivyo wengi wao kusepa hata kabla Bieber haja-perform!  

Ni asilimia 60 tu ya tiketi za show hiyo ya March 12 ndio zilikuwa zimeuzwa.

O2 Arena London, Justin Bieber alipiga show huku yiti vingi vikiwa vitupu!