Tanzania top model audition

Tanzania top model audition
Tanzania top model audition

Wednesday, 20 February 2013

OSCAR PISTORIUS ASHIKWA PABAYA MAHAKAMANI!

Ile kesi ya Oscar Pistorius, mkimbiaji riadha kwa kutumia miguu ya bandia, kutuhumiwa kumuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp siku ya Valentine imepata taswira mpya leo hii! Shahidi mmoja akitoa ushuhuda wake mahakamani jana alisema kuwa Oscar Pistorius alipomtungua  Reeva kwa bastola yake kwa maya ya kwanza, Reeva alisikika akilia, lakini Pistorius aliendelea kummiminia na kummiminia risasi!

Pistorius mahakamani

Oscar Pistorius na Reeva Steenkamp
Ikiwa bado masikilizano ya dhamani yakiendelea siku ya Jumatano shahidi mwingine alisema kuwa alisikia mlio wa risasi huku kukiwa na mwanga, mara akasikia mwanamke akilia kwa maumivu, na tena milio ya risasi iliendelea. Sasa hii ni tofauti na maelezo ya Pistorius aliyesema mahakamani kuwa alimpiga mtu (mpenzi wake) kukiwa na giza nene. Zaidi ya hapo bado upande mashtaka unasema kuwa upo ushahidi wa kuwepo kwa majibizano baina ya Pistoruis na Reeva kati ya saa nane na tisa usiku kabla ya mauaji.

Chooni ulipokutwa mwili wa marehemu Reeva Steenkamp
  
Ushahidi huu wote unamuweka Pistorius katika wakati mgumu zaidi hasa wa kupata dhamani kwa wakati huu.



SABABU YA KIFO CHA GOLDIE HIKI HAPA!

Ni muda sasa kukiwa na ukimya maradufu na sintofahamu kuhusiana na nini kilimuuwa msanii wa Nigeria Goldie. Sasa sababu ya umauti wake hadharani.

‘Stroke’ ama Kiharusi kilichosababishwa na kupanda kwa presha, High Blood Pressure au Hypertensive intracerebral hemorrhage kwa muda mrefu! Inasemekana Goldie aliathirika kwa muda mrefu. Hypertensive intracerebral hemorrhage ni aina ya Kiharusi inayosababisha kuvuja kwa damu kwenye ubongo!


NGULI WA FILAMU NIGERIA AFARIKI DUNIA!


Mwigizaji nguli wa maigizo ya filamu nchini Nigeria, Justus Esiri, 70, amefariki dunia. Jabali hili la filamu lilijizolea umaarufu mzito na kupewa jina la ‘headmaster’ kutokana na tamthiliya ya Village Headmaster mwaka 1980 ameiaga dunia jana usiku, February 19! 


Katika maisha yake ya uigizaji, Mzee Justus Esiri aliweza kujitwalia tunzo kadhaa zikiwemo THEMA Awards, NTA Honours Awards and AMAA Awards. Na baadhi ya filamu alizoigiza ni Wasted Years, Forever, The Prize, Six Demons, Corridors of Power, Last Knight, The Tyrant, The investigation, The Ghost

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na sababu ya kifo cha Mzee Justus Esiri.

RIP Justus Esiri

Monday, 18 February 2013

KIM KARDASHIAN APAGAWISHA NIGERIA

American favorite reality Tv star Kim kardashian a.k.a Mrs Kris Humphries ambaye very soon atakuwa mama wa mtoto wa Kanye West, yupo Lagos na sababu ya uwepo wake ni ku co-host concert ya Darey Alade, ‘Love Like A Movie’, Eko Hotel, jana usiku!



Hii ni mara ya kwanza kwa KK kwenda Nigeria na kama kawaida usiku huo alitokelezea na her favorite thing to wear toka aanze mahusiano na KW, kitu cha Leather! Na kuongezea na Black heels na make up ya wastani.



Kama ilivyotarajiwa na wengi ndivyo ilivyotokea. KK alifanya kile kilichotakiwa kufanywa na mtu wa level yake kwa kuipeleka concert international level!


BEYONCE: BLUE IVY NI NOMA!

Unaambiwa katika umri wa miezi13 mara nyingi watoto huanza kutambua taratibu vitu na watu wanaomzunguka tu. Hadithi ni nyingine kwa binti wa Beyonce na Jay Z, katika umri huo Blue Ivy herself ameshaanza mpaka kujua kusoma! 
 


Beyonce alisema hayo katika interview yake na Oprah Winfrey iliyokuwa inahusu documentary yake. “Ana akili sana. Ameshaanza kusoma maandishi katika vibao. Ni mzuri pia”. 



Vibao hivi mara nyingi hutumiwa na wazazi kwa ajili ya kuwafundishia watoto wao jinsi ya kusoma kwani licha ya kuwa na herufi pia zina picha.